Viongozi wa  Umoja wa Afrika wamemteua rais Robert Mugabe wa Kiongozi huyu mwenye miaka 90 amekabidhiwa  wadhifa  huo na  Rais wa Mauritania ,Mohamed Ould Abed Aziz ambaye alikuwa mwenyekiti hapo awali.
 Viongozi hao wa Afrika, wakiongozwa na rais wa Uganda Yoweri Museveni pia watajadilia mkakati  wa kujiondoa kwenye uwanachana wa Mahakama ya Kimataifa ya jinai-ICC. 
 Akizungumza na waandishi habari  hapo awali jijini Nairobi, rais huyo wa Uganda alisema “Mahakama  hiyo ya Wazungu inaendelea kuonyesha ujeuri na dharau kwa Waafrika.” Alisema ingawa ICC imeondoa kesi dhidi ya  rais wa  Kenya Uhuru Kenyatta, bado hajaridhika kwa sababu kesi dhidi ya Naibu rais wa Kenya William Ruto ingali inaendelea.
Wakati huo, huo viongozi hao wa Afrika wameidhinisha  mpango wa kupeleka kikosi cha pamoja cha wanajeshi 7,500 cha kukabiliana na  wanamgambo wa Boko Haram.
Hatua hiyo imefikiwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia Ijumaa . Nchi za Nigeria , Cameroon,Chad, Niger na Benin zilikubaliana kushirikana katika juhudi za kukabiliana na wanamgambo hao ambao wameua maelfu ya raia huko Nigeria na kujinyakulia  eneo kubwa la jimbo la Borno karibu na mpaka wa Cameroon na Chad.
30 Jan 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top