Na Hosea Mchopa #UO 1

Mvuto siku zote huleta ladha tofauti machoni pa watu na kukufanya uwe unatazamika zaidi na kuvutia watu wengi pengine zaidi ya kile ufanyacho.
Jose Mourinho


Siku hizi wanawake wanapenda sana soka kamwe usifikiri wanavutiwa na soka pekee bali ni vitu vingi huwafanya wawe wanafika viwanjani kila wiki.
mashabiki wanawake wa Crotia


Sahau kuhusu mwili wa Cristiano Ronaldo,tabasamu la Neymar na kifua cha Kelvin Prince Boateng pekee haviwafanyi hata wanawake wenye umri mkubwa kuhudhuria uwanjani.
Mchezaji mwenye mvuto duniani Cristiano Ronaldo

Geuka upande wa pili wa makocha wa timu nako utaona maajabu ya kwa nini wanawake wengi wanapenda soka siku hizi.
Mashabiki wanawake wa ujermani


Kuna makocha ambao wanavaa haswa,tena kwa staha na uchaguzi mzuri wa rangi unawaofanya wawe wa kipekee mbele ya watazamaji.

#UO inakuletea makocha tano ambao wamefundisha timu mbalimbali lakini katika upande wa fasheni wanaonekana kuiva zaidi.

1.JOSE MOURINHO

Hakuna ubishi kuwa ni moja ya makocha wenye mvuto wa kipekee katika ulimwengu wa soka akifahamika kama 'the special one'.

Kwenye mavazi kama hujui pia anaitwa the stylst one....Mourinho anajua kutupia haswa suti ambazo zinamfanya aonekana nadhifu kwelikweli.


Makoti marefu yaliyo na rangi nyeusi yakigandana na rangi yake nyeupe hufanya mashabiki wa kike wawe wanamtolea macho.

Na wa kiume kuangalia ubunifu wake na kuanza kuutumia.Bado ana miaka 52 akiinoa klabu ya Chelsea tutaendela kuona mengi kutoka kwake.

2.PAULO SOUSA

Nywele zake tangu anacheza soka katika timu ya taifa ya ureno zilikuwa gumzo kwa wadada zikiwa zinangara kwani hupaka mafuta sahihi haswa.

Mreno huyu anayeinoa FC Basel pia ni moja ya wanadamu wanaomanika kuwepo katika kikosi cha kizazi cha dhahabu cha ureno.

Si tabasamu pekee bali ni zile koti za Armani za kijivu zinazomfanya kuonekana tofauti kabisa na maridadi.

Alipofika Swanse idadi kubwa ya wanawake walikuwa rahisi kufahamu kam kuna mtu kaingia mjini kwao kwani alikuwa pekee sana.

3.PEP GUARDIOLA

Huyu ana miaka 44 baba wa watoto watatu Valentina,Maria na Mariaus.

Umbo lake linamfanya asipate shida sana kuchagua suti gani iwe halali kwa mwili wake na kuweza kutazamika kama kijana wa kipekee katika ya mashabiki maelfu.

Huyu huenda mbali muda mwingine hutupa kabisa suti na kuvaa vizibao vyenye rangi inaovutia huku akiwa na ugonjwa wa kuvaa saa za gharama.

Ukimuona huwezi kuuliza bosi wa eneo ni nani utamjua tu.

4.ROBERT MANCINI

Pamoja na kuzaliwa miaka 50 iliyopita huko Lesi,Italia bado Mancini yuko tofauti sana katika uchaguzi wa tai.

Sio lazima uvae tai nyeusi au nyekundu.Mancini anakuvalia nyeupe hata ya bluu na aliwafanya waingereza wengi waanze kuiba ubunifu wake mwingi alipotua Man city.

Anastahili kabisa kuonesha mavazi ya kampuni yoyote kwa sababu tayari mashabiki wanamtupia macho wakiiba ubunifu wake kila leo.

5LEONARDO ARUJO

Leonardo Nasciento de Araujo alizaliwa September 5 mwaka 1969 niteroi Brazil.Sasa ni director football wa klabu ya Paris Sain German pia aliwahi kuionoa Ac Milan na Inter.

Watafiti wa mambo wanaweka wazi kuwa huyu ndiye kocha handsome na mwenye mvuto na mwonekano mzuri a sura lakini anafunikwa na wengi kwenye kutupia tu.

Pamoja na hayo wataalamu wa ubunifu wanasema kama Leonardo asingekuwa kocha kwa jinsi anavyojali nywele zake na mwonekano wake.


Basi angeuwa mwanamitindo katika majirida ya play boy au mbunifu wa suti za wanaume.

Je katika nchi yetu ya Tanznaia makocha gani walikuja wakapita wakatuvutia kwa ubunifu wao wa mavazi au mwonekano na Papic au Patric Phiri au Jamhur Kihwelo Julio.

07 Apr 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top