Na Hosea Mchopa #UO 1

Basketball ni mmoja ya michezo ambao Inavutia watu wengi duniani kutokana na muundo wake na wachezaji warefu walio imara.Watu wengi wakiwa wanatazama mchezo huu huuangalia malighafi za jezi na aina ya viatu ambavyo wachezaji mahiri kama Le bron James huvaa.

Ili kukidhi haja yako mpenzi wa Basketball leo #UjumeOnline #OU kwa kutumia mitandao ya nje tumetatafiti juu ya viatu kumi ghali kabisa ambaVyo huvaliwa  na nyota katika mchezo wa Basketball.

10. Nike’s Air Force One
Air force I – Lebron Jame
Kiatu chenye mvuto wa kipekee ambacho nyota wa Basketball duniani Le Bron James anakitumia na mwaka 2014 nike walitengeneza sneaker maalumu kwa ajili ya Le Bron James.Bei ya kiatu hiki huendana na ubora wake ni karibu dola 2600 kwa pea.Rangi yake nyeusi iliyotawala kiatu na nyeupe  zinavutia sana zikichnagnywa na rangi nyekundu haswa iliyonakishiwa.
9. Air Jordan XI
Air Jordan XI
Kwa mara ya kwanza mwaka 1995 ndipo Air Jordan zilipoanza kuonekana duniani.Michael Jordan nyota wa kikapu duniani  alizitumia sana unakumbuka akivyoweza kuruka hewani na kutumbukiza mpira kwenye kikapu.Zimeboreshwa zaidi na sasa gharama yake ni dola 2800. Ni kiatu ambacho kina muonekano wa kuvutia na unakutofautisha na yeyote hakutazamae.
8. Golden KB8

Golden KB8
Ukizungumzia moja ya kiburi cha kampuni ya Adidas duniani ni Golden KB8.Ilikuwa mwaka 2004 ambapo kampuni ya Adidas walipoamua kutengeneza hivi viatu kwa ajili ya Kobe Bryant na jezi lake namba 8.Baada ya kuvaliwa na Kobe viatu vikawa maarufu duniani na kufikia gharama ya dola 3000.Kinachofanya ziwe ni za kipekee ni rangi yake ya njano kama dhahabu kinavaliwa sana na nyota wa Holywood
7. Air Jordan III
Air Jordan III

Tinker Hatfied ilimpasa awaze kwa akili ya ziada kuweza kufanya kazi ya kipekee kama hii.Air Jordan III zilianaza kuuza suara kwenye soko kwa mara ya kwanza mwaka 1988.Unakumbuka logo ya Nike Air ilikuwa inapamba kwa mara ya kwanza.Mchezaji Nguli wa Basketball anakiri kuwa viatu hivi ni vizuri sana.Gharama yake ni dola

6. Air Jordan VII

Air Jordan VII – Olympic 1992
Air Jordan VII ubunifu mwingne wa kipekee uliotumika kuumba na kukitengeneza kiatu hiki.Mwaka 1992 kilivaliwa sana katika msahindano ya Olimpic ndipo wadau wa Basketball tukaanza kuvutiwa sana.Kina bei ya juu sana ili kukimiliki inahaitaji pochi yako iwe na dola 72000.

5. Air Jordan VI
Air Jordan VI


Una kiasi gani unataka kiatu kizuri cha Basketball.Air Jordani VI si rahisi kukimiliki itakulazimu utoe dola 7500 huweze kupata kiatu hiki.Unakumbuka mechi ya Bulls alipomfunga Lakers na kuchukua ubingwa Michae Jordan alikuwa anakikanyaga ardhini.

4. Air Jordan I – Original Version

Air Jordan Original
.Kwa mara ya kwanza kilianza kung’arisha maduka ya watu mwaka 1985.Ni kiatu kizuri na cha kipekee kwa mwanamichezo kuweza kukivaa.Dola 8000 ndio itakayokuwezesha kukipata kiatu halisi cha Air Jordan.

3. Air Jordan V


Air Jordan V
Ni kama Air Jordan XI hapa picha ya Michael Jordan akitumbiza mpira kikapuni utaiona kwa nyuma.Zilitoka matoleo mengi lakini la namba 23 lilikuwa kiboko,ndio mana wakaamua dola 10000 ziamue umiliki wa kiatu hiki.
2. Air Mag
Nike Air Mag
Waaaoh ! unaweza ukajikuta unashangaa pale ukimwona Michael J Fox akiwa amevaa Nike Air Mag.Vina mvuto kwelikweli ni viatu vya daraja la juu duniani.Ili uweze kuonekana wa kisasa zaidi lazima apunguze katika akaunti yako dola 12000 kuweza kununua kiatu cha kipekee.
1. Air Jordan I –

Air Jordan I – 
Rangi nyekundu isiyochubuka kirahisi ikiwa imenakishiwa karibu na rangi nyeupe hufanya macho kupata burudani ya kipekee.Air Jordan 1 ni nambari moja hakika kinastahili kuwa kiatu cha gharamA katika ulimwengu wa Basketball.Ili uweze kukipata itakulazima kutunza kiasi kidogokidogo kwenye akaunti yako mpaka zifike dolla 25000 kamili ndipo ukajitwalie.


21 Feb 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top