Na Hosea Mchopa #UO 1

.Hii si habari kubwa kwenye ulimwengu wa Mario Balotelli,hata akiangalia video ya Steven Gerrad akimkosoa anaweza akapata kicheko kikali.Kipi Mario kinamumiza kichwa kama anasakamwa na dunia nzima kumwacha mama yake aishi katika maisha ya kawaida wakati yeye akichezea madola.

Mama yake mzazi Rose Barwuah anatazama maisha ya kimilionea ya mwanae wa kumzaa kama wewe unavyotazama.Mama yake anaishi maisha ya kawaida kabisa Wythenshaw pale Manchester.Mama yake kwa upendo alionao kwa Mario alihamia mjini Manchester ili kuwa kwa karibu na mwanae kujenga mahusiano bora baada ya Mario kuhamia Manchester City.
Familia nzima ya Mario Barwuah Ballotelli


Mama yake Mario Balotelli amezoea shida kama waafrika wengine wanavyoishi ulaya.Anatengeneza pesa kwa kufanya usafi kwenye majumba ya watu na popote pale penye uhakika wa kumuingizia pesa.

Wakati Mario Ballotelli anaishi kwa kufanya chochote apendacho katika dunia hii akiendesha Ferrari F12 Berlineta lenye gharama ya paun 240,000.Muda wa chakula ukifika ana uwezo wa kwenda kula mighahawa ya gharama katika jiji la Liverpool.Mama yake bado anapanda mabasi ya abiria na mahitaji yake anachukua maduka ya kawaida kabisa.


Mama yake Rose na dada yake mwenye maiaka 15 Angel wanaishi kawaida sana wanachohitaji ni upendo tu kutoka kwa damu yao.Pesa zake sio kitu muhimu katika maisha yao.Enoche ndio binadamu pekee ambaye Mario Balotelli uwa nae karibu ambaye  anacheza katika klabu ya Vallecamonica.
Balotelli na Enoche wakifurahi picha
Balotelli akiwa na Enoche enzi za utoto wao




Mario Balotelli damu yake tu ndio ya mzee Thomas Barwuah na Rose Barwuah lakini yeye ni mali  halali ya Silvio na Francesco Balotelli waliyekabidhiwa akiwa na miaka 2.Na kuishi nao huku siku za jumapili akipata nafasi ya kujumiaka na Enoche na familia kwa ujumla.Mario alilelewa kwa heri na wazazi wake hadi hali yake ilipokuwa mbaya ikabidi wazazi watafute sehemu itakayokuwa inampa uhakika wa kuweza kuishi maana daktari alisema anaweza akapoteza maisha.
Mario Balotelli akia na mdogo wake Enoche na mama yao Rose Barwuah

Ushahidi wa picha za pamoja unaonesha Mzee Barwuah hakumtupa na wala haitaji pesa zake kama Mario alitomka.Anakumbuka tabasamu lake udogoni akicheza mpira katika mvua na kumwita Super Mario.Na sasa akiwa Mario mwingine kabisa anayeamini pesa ndizo zinaifanya famillia imkumbuke japo kwa sasa anajirudi kiasi.Hii si habari kwangu na wala haitaingia katika kumi bora zangu za Mario nitakumbua hivi tu.
Balotelli akiwa na wazazi wake waliomwasili Silvio na Francesco



Ilikuwa dakika ya 85 mechi kali ya kombe la  ulaya kati Liverpool na Besktas.Mwanaume mwenye kilo 86.17 anachukua mpira na kwenda kupiga penati pasipo nahodha wa timu Hendo kumruhusu kwa moyo mkunjufu.Anafunga  penati na kuipa matokeo Liverpool matokeo muhimu  katika uwanja wa Anfield.
Mario Balotelli akijiandaa kupiga penati

Hana shaka lolote katika hii sayari mawazo yake yako haraka kufanya maamuzi ya ajabu ambayo kwake yanakua sahihi kwa huo mda.Unakumbuka alipomuuliza mdogo wake Noche unataka kuona wafungwa.Na ghafla akaelekeza gari ndani katika  gereza la wanawake Italia.

Manung’uniko humalizwa na furaha,na hakuna furaha tamu kama ile ya kushitukizwa.Henderson Jordan alisahau kama Super Mario alifanya kosa.Furaha hii imefanya mashabiki wa Liverpool wasielewe kabisa lugha anayoongea kipenzi chao cha miaka mingi Steven Gerrad.
Balotelli akishangilia baada ya kufunga peanti dakika ya 85


Steven Gerrad akiongea katika kituo cha televisheni Uingereza ITV aliongea kwa msimamo kuwa Mario Balloteli ameonesha kitendo cha utovu wa nidhamu kwa Jordan Henderson.Gerrad alichukizwa na kitendo cha Mario Balloteli kwenda kupiga penati na kumpora mpira Henderson wakati alikuwa tayari kwenda kupiga penati.

Kocha Brendan Rogers kwa upande wake yeye alisema ni matokeo mazuri na wanajipanga kwa mchezo wa marudiano.Hakuwa na pingamizi kwa yaliyotokea matokeo ya ushindi ndiyo yalikuwa jambo la muhimu kwake.
Moja ya magari yanayomilikiwa na Mario Ferrari F2

Ingawa baadae akiongea na waandishi wa Habari katika maandalizi ya mchezo wa jumapili alisema hakupendezwa na namna wachezaji wake walivyokuwa wanamgogoro juu ya nani atapiga penati.Henderson ndiye alimpanga mbadala wa Gerrad kupiga penati katika kikosi kilichoanza.

Kwa kawaida kama Gerrad,Henderson na Mario wapo ndani wote wameanza.Mario na Gerrad ndio huwa wananafasi kubwa ya kupiga penati.Kwa kuwa Mario hakuanza mechi basi Henderson ndiye alistahili kupiga penati.

 Pamoja na haya hakuna cha kupoteza katika maisha ya Mario Balotelli amefunga goli lake la nne kwa msimu na la pili kwa kombe la ulaya.Ametengenza historia tamu ya kipekee kufunga penati 26 kati ya 28 alizopiga.

Jordan Henderson ambaye alikuwa kiongozi wa wachezaji katika mechi hiyo.Alikiri kuwa alihitaji kupiga penati.Lakini Super Mario alionesha kujiamini na yeye akaweka imani kwa Mario kwani anahistoria kubwa katika kupiga penati.
Balotelli akifunga penati dhidi ya Beskitas


Mario Balotelli ambaye kwa sasa yupo karibu sana na mashabikiwa Liverpool katika mitandanao ya kijamii baada ya mechi hiyo.Aliandika ujumbe wa kumshukuru Jordan Henderson ‘Hendo’ kwa kumwacha akapige penati na kuwataka mashabiki wa Liverpool kuacha kuendeleza filamu ambayo haina faida kwao.

Hili ni jambo dogo sana kwa Super Mario Balotelli tena hata faini hajapigwa.Wakati akiwa Manchester city aliwahi kuvunja sheria aliyoweka kocha wa wakati huo Robert Mancini ya kutomruhusu mchezaji yeyote kwenda mjini  kujirusha masaa 48 kabla ya mechi.

Mario Balotelli akiwa na rafiki zake walijumuika katika klabu ya usiku na akapigwa faini ya dola 400,000.Na wala hakuwaza kama  tatizo katika ubongo wake aliona ni jambo dogo katika ulimwengu wake.

Yeye aliweka hadharani vile ambavyo wengine walificha na wala hakuona tatizo.Februari 12 alipofunga goli alionesha fulana lililoandikwa nakupenda Raffaela .Huyu ni msichana maarufu huku nchini Italia ni mwanamitindo na anakashifa mbaya ya kushiriki katika sherehe za Bunga Bunga ambazo Silvio Berluscon huziandaa kwa siri.
Balotelli akimpa ujumbe mpenzi wake Raffaela


Unakumbuka kituko chake cha mwaka 2012 aliposimama katika shule moja mtaani huko Uingereza na kwenda kujisadia katika vyoo vya wanafunzi.Bila kujali jina lake baada ya kumaliza haja zake akiwa na rafiki zaake aliwasha gari lake la Bentley na kutokomea.

Ni binadamu aliyekuwa akiwaza tofauti na wengine kabisa alipokuwa katika klabu ya Manchester City.Alipigwa faini ya dola 100,000 baada ya kukutwa akicheza mchezo wa kurusha vishale(darts) na timu ya vijana wadogo.Alipoulizwa sababu ya kufanya hivyo alisema alihisi upweke.

Ni mwafrika mwenye jeuri na rangi yake anajua anafuatwa na vyombo vya habari kila anapokanyaga.Alitengenza habari kubwa april 2011 alipompa kijana asiye na kazi dola 1000 baada ya kushinda mchezo wa kamari dola 250000 katika Casino.


Ana ushawishi mkubwa katika upande wa michezo ya video(video game) kwa kikatuni kinachojulikana na jina la Super Mario kimeonekana katika game 200.Na ameuza zaid ya millionI 193 ya michezo ambayo yeye yumo.Jina ake limepelekea hili jina la Super Mario kuwa na ushawishi mkubwa

Ni habari ndogo sana kwake Mario ukizangatia ni jambo ambalo halijathiri klabu yake ya Liverpool zaidi ya kuleta faida.Sasa hivi atakuwa amekaa pembezoni mwa nyumba yake akiwa na glasi ya wine akitabasamu kila akiona kurasa za nyuma zikitokea na jina lake.

Thomas Barwuah baba mazazi wa Balotelli



22 Feb 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top