Na Azard Mpango
Rais wa zamani wa Nigeria ambaye ni mwanajeshi mstaafu
aliyeishia cheo cha Luteni Jenerali, Olesegun Mathew Obasanjo aliyezaliwa Machi
5, 1937 katika eneo la Abeokuta nchini Nigeria, ameamua kuongea kwa vitendo
kuwa ameachana rasmi na siasa za Nigeria.
Obasanjo ambaye aliiongoza nchi yake kwa awamu mbili
tofauti, awamu ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1976 mpaka 197n akiwa Rais wa kijeshi
aliyeteuliwa na Halmashauri ya Kijeshi na baadaye akaitisha uchaguzi wa kiraia
ambapo Shehu Shagari alishinda na kuwa Rais mpya wa Nigeria.
Awamu ya pili ya Obasanjo ilikuwa ni mwaka 1999 mpaka 2007,
ambapo alichaguliwa na wananchi kupitia chama cha People's Democratic Party
(PDP). PDP ndicho chama tawala nchini Nigeria kinachoongozwa na Rais wa sasa
Goodluck Jonathan anayegombea kwa awamu ya pili kwenye uchaguizi unaotarajiwa
kufanyika mwezi Machi mwaka huu.
Mara nyingi mzee Obasanjo amelaumiwa kuwa hayuko pamoja na
PDP, chama ambacho alikuwa kiongozi wa chama hicho katika cha urais wake wa
awamu ya pili. Alinyooshewa vidole na ilifikia hatua kuonekana ni mpinzani hasa
katika uongozi wa Rais Jonathan.
Rais Jonathan ni miongoni mwa waliomlaumu Obasanjo kwamba
anakipigia debe chama kikuu cha upinzani cha All Progressive Congress (APC)
kinachowakilishwa na Muhammadu Buhari hali inayomkatisha tamaa Rais Jonathan
kwa sababu Rais mstaafu alitakiwa aokoe jahazi la PDP.
Obasanjo aliyejiunga na jeshi la Nigeria mwaka 1958 kama
vile hakuwa na jibu la kuwapa wanaomlaumu kuunga mkono upinzani kwa sababu
sauti yake iliwahi kusikika ikiahidi kuwa hatoweza kuachana na PDP na kama ikitokea
basi hatajiunga na chama kingine.
Kwa kuwa Rais huyo mstaafu aliyepata kufungwa jela na
kiongozi wa kijeshi Sani Abacha kati ya mwaka 1995 na 1998, hakueleweka vyema
amerudia ahadi yake kuhusu PDP tena safari hii alikuwa akizungumza na viongozi
wa chama hicho kutoka kata 11 waliomtembelea katika makazi yake ya Hilltop
yaliyopo Abeokuta Kaskazini, nchini Nigeria.
"Niliwahi kuwaambia kuwa nilikuwa Rais kwa jukwaa la
PDP, kwa heshima yake nikiondoka sitajiunga na chama kingine. Nitabakia
Mnigeria wa kawaida, nipo tayari kufanyakazi na yeyote bila ya kujali itikadi
yake ya kisiasa," Obasanjo aliwaambia wanachama hao.
Mzee Obasanjo hakuishia maneno hayo tu bali alitangaza rasmi
kuachana na siasa na alichana kadi yake ya uanachama mbele ya viongozi wa PDP
huku kabla ya kufanya jambo hilo gumu aliorodhesha mlolongo wa udhaifu wa
Serikali ya Rais Jonathan.
Kwa kuchana kadi yake ya uanachama, tukio lililotokea
katikati ya mwezi Februari mwaka huu, Obasanjo sio mwanachama wa PDP lakini
alisisitiza kutojiunga na chama chochote. Kwa hatua hiyo bila shaka Rais huyo
mstaafu ambaye alinusurika kuuawa na wapinzani nadi ya jeshi ni ishara kwamba
amevunja ukimya na ameamua kujitenga na mikikimikiki ya siasa.
Hebu tujifikirishe kidogo! Mfano kitendo alichofanya mzee
Obasanjo cha kuchana kadi ya chama, angekifanya 'Mzee wa Ruksa', Rais mstaafu
Ali Hassan Mwinyi au 'Mr. Clean' Benjamin Mkapa, ingekuaje? Wananchi na
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wangesemaje?
Mkapa ambaye hakuonekana katika sherehe za makabidhiano ya
Katiba Inayopendekezwa, imekuwa nongwa, vipi akichana kadi ya CCM? Leo
analaumiwa na baadhi ya wananchi kwamba amejitenga mno na uongozi wa awamu ya
nne, itakuwaje siku atakapotaja udhaifu wa Serikali iliyopo kama alivyojiamua
Obasanjo? 'Kupumzika kama Obasanjo sio dhambi'
0 maoni:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.