KLABU
YA SOKA YA YANGA YA DAR ES SALAAM NA
MAJI MAJI YA SONGEA ZIMECHUANA VIKALI KATIKA UWANJA WA MAJIMAJI MJINI SONGEA
AMBAPO TIMU YA YANGA IMEIBUKA NA USHINDI WA BAO
MOJA KWA SIFURI.
BAO HILO LA YANGA
LIMEFUNGWA KATIKA DAKIKA YA KUMI NA TATU
NA DEUS KASEKE BAADA YA MABEKI WA MAJI MAJI KUSHINDWA KUMZUIA HADI KIPINDI
CHA KWANZA KINAMALIZIKA YANGA ILIENDA
MAPUMZIKONI IKIONGOZA KWA BAO HILO MOJA.
KATIKA KIPINDI CHA
PILI TIMU HIZO ZILISHAMBULIANA KWA ZAMU HUKU MAJI MAJI IKIKOSA BAO LA WAZI
KATIKA DAKIKA YA 36 KIPINDI CHA PILI
AMBAPO ULINZI MKALI ULIKUWA UMEIMARISHWA KATIKA UWANJA WA MAJI MAJI HUKU TIMU
YA YANGA IKIGOMA KUINGIA KWENYE VYUMBA
VYA KUPUMZIKIA NA KUINGIA UWANJANI
WAKITOKEA KWENYE GARI LAO.
0 maoni:
Chapisha Maoni