SIKU CHACHE BAADA YA KUPATA USHINDI MNONO WA GOLI 3-0 DHIDI
YA WANALIZOMBE MAJIMAJI MUJJARAB MWENYEKITI
KAMATI YA USAJILI YA SIMBA ZACHARIA HANSPOPE AMEWATETEA BAADHI YA WACHEZAJI
WALIYODAIWA KUSHUKA KIWANGO.
HANS POPE AMESEMA BADO HAJAONA UZITO WA KAULI HIYO KWANI
IMEKOSA USHAHIDI NA TAKWIMU KAMA SIMBA INGEKUWA IMEFANYA USAJILI MBAYA
WASINGEWEZA KUONGOZA LIGI KWA MUDA MREFU HUKU BADO IKISALIA NAFASI YA PILI TENA
KWA PUNGUFU YA ALAMA 1.
MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI WA SIMBA AMESEMA HUU NDIO
MSIMU AMBAO KLABU YA SIMBA IMEKUWA KATIKA KIWANGO CHENYE UWIANO MZURI PAMOJA
NA KUWA SAFU YA USHAMBULIAJI AMBAYO ILISHINDWA KULETA MATOKEO MAKUBWA AMBAYO
AMEITETEA KUWA HUENDA MFUMO WA KOCHA NDIO UNAWEZA KUWAFANYA WACHEZAJI HAO
KUFANYA VIZURI.
![]() |
Zacharia Hans Pope |
0 maoni:
Chapisha Maoni