AMA
HAKIKA MABANGO YA WHITE CHIRSTMAS YA MASHABIKI WA REAL MADRID
YATAKUWA MAZITO BAADA YA WANAJESHI WA CATALUNYA KUVAMIA HIMAYA YA MADRID NA
KUWATEKETEzA KIKATILI TENA WAKIZITUMIA VYEMA DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA PILI.
NI LUIS SUAREZ DAKIKA YA 54,LIONEL MESSI KWA
MKWAJU PENATI DAKIKA YA 64 NA ALEX VIDAL DAKIKA YA 90+3 NDIO WALIOBADILI
SIMULIZI YA REAL MADRID KUOMBA GWARIDE YA HESHIMA BAADA YA KULINUA TAIFA LA
ULAYA KWA KUTWAA MARA MBILI MFULULIZO MASHINDANO YA KLABU BINGWA DUNIA HUKO ABU
DHABI.
![]() |
Wachezaji wa Barcelona wakishangilia goli dhidi ya Real Madrid |
BAADA
YA MATOKEO YA LEO REAL MADRID WAKO NAFASI YA NNE WAKIACHWA KWA ALAMA 14 NA
BARCELONA WENYE ALAMA 45 NA MICHEZO 17 WAKATI REAL MADRID ANA ALAMA 31 NA
MICHEZO 16 .INGAWA BARCELONA ANAMUACHA ATLETICO MADRID ALIYE ANAFASI YA PILI
KWA ALAMA 9 ,ATLETICO WAKIVUNA ALAMA 36.
MAKOCHA
WOTE WAKITUMIA MFUMO WA 4-4-2 LAKINI MAAJABU YALIKUWA KWA ZINEDINE ZIDANE AMBAYE
ALIWANZISHA VIUNGO WAKE MATEO KOVASIC,CASEMIRO,LUKA MODRIC NA TON KROOS PAMOJA
AMBAO WALIWAFANYA SERGIO BUSQUET,PAULINHO ,INIESTA NA RACTIC WAIFANYE LOLOTE
KIPINDI CHA KWANZA HADI KATIKA UPIGAJI WA PASI ZA UHAKIKA KIPINDI CHA KWANZA WAKIZIDIWA KWA ASILIMIA 84
KWA 87.
![]() |
Wachezaji wa Real Madrid wakionekana kupigwa butwaa baada ya goli za haraka haraka za Barcelona |
REAL
MADRID WALISHINDWA KUZITUMIA VYEMA NAFASI WALIZOPATA KIPINDI CHA KWANZA UKIACHA
GOLI LILILOKATALIWA NA MWAMUZI LA CRISTIANO RONALDO,HUKU KARIM BENZEMA AKIKOSA
NAFASI ZA WAZI NA BAADAYE ALITOLEWA BAADA YA CARVAJAL KUPEWA KADI NYEKUNDU NA
NAFASI YAKE IKACHUKULIWA NA NACHO.
KIPINDI
CHA PILI KOCHA WA BARCELONA VALVERDE ALIUTEGEU MTEGO WA ZIADNE NDIPO WAKAANZA
KUWAPOZA NA KUWASHAMBULIWA KWA KUSHITUKIZA NA KUPATA BAO LA KWANZA KUPITIA KWA
SUAREZ.NDIPO KOCHA ZIDANE AKAWASIMAMISHA WACHEZAJI WAKE WATATU GARETH
BALE,ASENSIO NA VAZQUEZ ILI WAPASHE MISULI LAKINI MAHESABU YAKE YALIHARIBIKA
BAADA YA CARVAAL KUPATA KADI NYEKUNDU HIVYO
ALIMTOA CASEMIRO DAKIKA YA 62 NA KUMUINGIZA ASENSIO NA AKAMTOA KOVACIC
DAKIKA YA 72 NA KUMUINGIZA GARETH BALE.
![]() |
Ronaldo akifunga goli kwa kichwa |
WAKATI
BARCELONA AKINGIZWA GOMEZI KUCHUKUA NAFASI YA PAULINHO DAKIKA YA 84 NA SEMEDO
KUCHUKUA NAFASI YA INIESTA DAKIKA YA 77
MUDA
MFUPI NITAKULETE REKODI YA WAPINZANI HAWA.
![]() |
Mapema Nahodha Sergio Ramos alionesha kombe la klabu bingwa dunia waliloshinda huko ABU DHABI |
0 maoni:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.