Na hosea Mchopa

Klabu ya West Ham imethibitisha mshambuliaji wake Andy Carroll atafanyiwa upasuaji wa goti siku ya jumanne baada ya kufanyiwa vipimo ijumaa mchana.

Carroll mwenye miaka 26 ambaye pia ni mshambulaiji wa timu ya taifa ya Uingereza aliumia jumatano wakati timu yake ilipotoka sare ya tasa na klabu ya Southmpton katika dimba la St Marry


Andy Carroll ambaye alianza maisha yake ya soka la kulipwa katika klabu ya Newcastle  upasuaji atakaofanyiwa utamlazimu kukaa nje kwa msimu mzima uliobakia.

Kubwa kutoka kwa Carroll
Carrol msimu wa mwaka 2011 siku ya mwisho ya dirisha la usajili tarehe 31 januari  aliuzwa na klabu ya Newcastle kwenda Liverpool kwa ada ya paun milioni 35,kabla ya kupelekwa West Ham kwa mkopo kwa ada ya paun milioni 2.
June 2013 West ham walimchukua jumla kwa ada ya pauni milioni 15.


Takwimu za Andy Carroll 2014-2015
Mechi-14
Goli-5
Pasi ya goli-1

Kadi za njano-2

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top