Na hosea Mchopa
Mchezaji hatari wa klabu ya Chelsea Eden Hazard amekubali kuongeza
mkataba wa miaka mitano kukipiga katika klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu
nchini Uingereza.
‘Tangu nimekuja hapa mwaka 2012,Kila mara nimekuwa vizuri na
klabu imekuwa ikinipa mchango mkubwa kwangu’alisema Eden Hazard

Mkataba huu utamfanya Eden Hazard mwenye miaka 24 kukaa
darajani hadi mwaka 2020.Na kuweza kudhihirisha uwezo wake katika ligi kuu ya
uingereza.
‘Ni kijana mdogo na anaweza kuwa mchezaji bora’Kauli ya
kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho
Mkataba wa Eden Hazard ambaye anaingiza karibu pauni 200,000
kwa wiki utagharimu pauni milioni 57.
Mafanikio yake
Hizi ndizo idadi ya mechi na magoli ya Eden Hazard ambaye
wataalamu wa soka wanamtabiria kuja kuishika dunia ya soka miaka ijayo.
Katika klabu ya Lille OSC mechi 194 magoli 50
Klabu ya Chelsea mechi 147 magoli 44
Mataji Ligue 1
mwaka 2010-2011
Couple de France 2010-2011
UEFA Europa ligi 2012-2013
0 maoni:
Chapisha Maoni