Na.Hosea Mchopa

Unataka mkataba mnono,unataka kupandishiwa mshahara katika soka hakuna binadamu mwingine wa kumtafuta zaidi ya Jorge Paulo Agostinho Mendes.Ana nguvu ya ushawishi katika ulimwengu wa soka.

Sasa yuko makini na Manchester united wakiangalia maslahi mapya ya mteja wake David De gea.Wakipindisha maneno hataona tabu kuhamishia meza yake Santiago Bernabeu kuitikisa duniani ya soka.

Majibu yake mafupi yaliyojijitosheleza hudhihirisha jinsi gani analinda na kuwasimamia wateja wake .Ana jicho la Tatu kuweza kuona thamani ya mchezaji kirahisi kuliko kawaida.

Jose Mourinho ilimpasa kumbwaga wakala wake Jorge Baidek na kusaini kwa Mendes ambapo mwaka 20004 akajiunga na Chelsea.Jorge Mendes akisimamia mpango mzima wa uhamisho huo.

‘Bila mjadala Jorge Mendes ni wakala bora kuwahi kufanya nae kazi, ,Aliwajibika na anatenda haki kwa klabu’.Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester united Sir Alex Ferguson alinukuliwa akimpongeza wakala Mendes ambaye alisimamia mpango wa Ronaldo kuhamia Real Madrid na kuvunja rekodi ya usajili.

Jorge Mendes katikakati akiwa na wateja wake Josse Mourinho kulia na Christiano Ronaldo

Mawakala wetu watatu nchini Tanzania ambao wanatambulika na FIFA John Ndumbaro,Ali Salehe na Mehdi Remtulla wanahitaji kumtazama Mendes.Utashindwajwe kumtia Mkude mikononi ukamuuza Afrika ya kusini wakati Mendes alimuuza Bebe Manchester united bila Alex Ferguson kumuona.

Mendes hucheza na akili za watu katika biashara anajua ujanja wa bashara katika soka .Bebe kutoka mikono ya wakala wake Goncalo Reis hadi kwa Mendes.Na kumfanya Mendes kuweka kibindoni paun milioni 3.6 katika uhamisho wake kutoka Vicktoria Guimaraes kwenda United kwa ada ya uhamisho pauni milioni 9.

Ukiwataja mawakala hodari 12 wa michezo yote duniani waliofanya mikataba ya minono .Hapa itakupasa  kumsahau kabisa Jorge Mendes na kumtaja Scot Boras.Boras mtaalamu ambaye amesomea mambo ya mikataba na sheria katika chuo cha Mc George.

Dunia inamkumbuka Boars  mwaka 2007 kwa  kusimamia mpango wa uhamisho dola milioni 275 kwa mkataba wa miaka 10 wa Alex Rodriguez  ‘A Road’ wa timu ya baseball ya New York Yankee ya ligi kuu ya Baseball nchini Marekani.

Boras biashara zake nne kubwa katika ulimwengu wa baseball  amefikisha dola million 701 na kuitikisa dunia ya michezo.Kumbuka alivyosimamia mauzo ya Alex Rodriguez dola milioni 275,Max Teixeteira dola million 180,Bary Zito dola million  126 na Mat Holliday dola million 120.

Lakini ulimwengu wa Soka pamoja na uwepo wa mawakala hatari kama Mino Raiola,Jonathan Barnet aliyepiga biashara kubwa ya uhamisho wa Gareth Bale.
Mtaalamu wa dirisha la usajili Jorge Mendes anatawala kwa kuwa na uwajibikaji kwa mchezaji wake hadi kufikia hatua Cristiano Ronaldo alimwita ni wakala muwazi na mwenye haki.

Jorge Mendes toka kuwa dj na kumiliki klabu ya usiku mpaka kuwaza kulishika soka kwa kuanza kufanya biashara yake ya kwanza ya mchezaji wa kireno Nuno kutoka Victor de Guimaracia kwenda Deportivo la Coruna mwaka 1996.

Kutoka biashara ya kwanza nono kimataifa katika kazi yake ya uwakala wa  soka kwa kuuza Hugo Viana kutoka Sporting CP kwenda Newcastle united kwa ada ya euro million 12.

Mpaka kuitikisa duniani kwa kufanya biashara ya kumuuza Cristiano Ronaldo kwenda Real Madrid kwa ada ya euro million 80 huku ikiripotiwa Mendes akiweka kibindoni euro million 4.Jorge Mendes anaiendesha dunia ya soka kwa kufanya biashara zenye kuvutia na kucheza na tarehe za mwisho wa dirisha la usajili.

Kwa mwaka 2014 katika usajili ameingiza paun million 30.Amefanya biashara ya James Ridriguez kutoka Monaco kwenda Atletico Madrid kwa ada ya paun million 63,Angel Di Maria kutoka Real Madrid kwenda Manchester united kwa ada ya pauni million 60.
Mendes pia alifanya biasahara ya kumtoa Diego Costa kutoka Atletico Madrid kwenda Chelsea kwa ada ya pauni million 32 na Eliaquam Mangala kutoka Fc Porto kwenda Manchester City kwa pauni million 32.

Kuna watu wanawasaini mkataba na wachezaji na wanasubiri Jorge Mendes kuwaonyesha kwa watu na kuwapeleka kwenye klabu kuwa.Anaweza kufanya chochote sasa mwaka 2012 nusu ya kikosi cha timu ya taifa ya ureno kilikuwa na wateja wake.
Diego Costa,Yacine Brahim,Jose Mourinho,Luiz Felipe Scorali,Carlos Quieroz,Simao Sabrossa,Anderson,Fabio Coentrao,Pepe,Angel di Maria,Cristiano Ronaldo,Radamel Falcao,Ricardo Cavarliho,,Luis Nanni,Ricardo Quaresmaa,Joao Moutinho,James Rodriguez,David de gea na Victor Valdes ni moja ya watu wanaopata huduma ya Jorge Mendes.c


13 Feb 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top