Serikali ya Liberia imeahidi kufungua mipaka yake na nchi jirani kuanzia kesho Jumapili.
Aidha Rais Ellen Johnson Sirleaf wa nchi hiyo amekubaliana na pendekezo la kufunguliwa vivuko vya mipaka ya nchi hiyo ambavyo vilifungwa mwaka jana kwa lengo la kuzuia maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola .
sambamba na kutangaza kufutwa amri ya kutotoka nje. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hatua hiyo itatekelezwa kuanzia kesho tarehe 22 Februari.
Virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola vilienea kwa kasi sana mwaka jana 2014 katika nchi za Guinea Conakry, Sierra Leone na Liberia na kupelekea maelfu ya watu kupoteza maisha huku makumi ya maelfu ya wengine wakiwa wameambukizwa maradhi hayo.
Rais wa Liberia Ellen Johson Sirleaf
0 maoni:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.