#news room
Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, Jamal Benomar amesema kuwa, Harakati ya Answarullah na makundi tofauti ya kisiasa yamekubali kuunda serikali ya kisheria katika kipindi hiki cha mpito.


Benomar ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Intaneti na kuongeza kuwa, makubaliano hayo yamefikiwa kwa ajili ya kuyashirikisha makundi ya kisiasa ambayo hayakuhusishwa katika baraza la wawakilishi la hivi sasa. 

Aidha amesema kuwa, baraza hilo litaendelea na kazi zake na kwamba mbali na baraza hilo kutaundwa pia baraza jingine litakaloitwa Baraza la Wananchi la Mpito litakaloijumuisha mirengo mbalimbali ya kisiasa baraza ambalo pia litaipatia eneo la kusini asilimia 50 ya viti. 

Kwa mujibu wa mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, Baraza la Wananchi la Mpito litakuwa na uwezo wa kutunga sheria katika kipindi hiki cha mpito. Hayo yanajiri katika hali ambayo nchi mbalimbali zingali zinaendeleza njama, mashinikizo na vitisho dhidi ya Harakati ya Answarullah, kwa lengo la kuiondoa harakati hiyo katika ulingo wa kisiasa nchini Yemen.

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top