Toleo la 1
Na Hosea Mchopa #UO 1
Katika ardhi ambayo inafanya historia ya Tanzania kuwa tamu
na ya kipekee duniani kwa kuwa na mto uliotengenesha na nchi ya Msumbiji.Ardhi
iliyoleta jina la majimaji katika ulimwengu wa historia ya vita vya kugombania
uhuru katika nchi ya Tanganyika.
Nikikutana na binadamu wacheshi wenye rangi kama yangu nyeusi
kwa pamoja tukiwakilisha rangi nyeusi ya bendera yetu.Nikakutana na
wamatengo,wayao,wandendeule,wabena,wangoni,wamakua na wandegereko.
Ama kweli Afrika ni asili tamu kuwahi kuifahamu.Ardhi ambayo
inakubwa wa kilomita 63,498 na wakazi
1,117,166 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2002.Majumba ya asili ya kizamani
inafanya ujue ni afrika huku maduka mengi yakijihusisha na uuzaji wa
madini.Kuthibitisha neema ya mungu ya kuijaza Afrika vitu vya thamani.
Huu ni mkoa wa Ruvuma wenye wilaya sita ulionipa siri ambayo
ni dhahabu serikali ya Ruvuma inahitajika kuitafiti zaidi.Nikitokea moja kwa
moja katika moja ya mikoa midogo Tanzania mtwara wenye kilomita 16,720.
Urefu wa safari haukuwa ni tatizo kwangu nilihitaji kujifunza
mambo mengi mapya maisha mwangu nikiwa nina sura nyingine.Sura ya kuiandika
nchi yangu Tanzania popote pale nitakapokanyaga kwani naamini tumebarikiwa
vingi.
Mwenye Mpelia Kamtande katika kijiji cha Mtonya aliweza
kuingia katika historia yangu kwa kunipa siri ya mlima Chamanga ambao ni rahisi kuonekana na
kuufikia ukiwa katika kijiji cha Mtonya.
Nikifuatana na mwenyekiti wa kijiji na watu wa karibu wa
kijijini nilipelekwa moja kwa moja kwa mzee Mwenye mpelia.Yeye alinipa utofauti
mkubwa uliopo kati ya mlima wa Chamanga na milima mingine ninayoiona.
Mlima huu una maajabu ambayo yakiangaliwa na serikali unaweza
ukawa chanzo cha mapato kwa wanakijiji ambao wanategemea kilimo pekee.Kwani
watafiti wakijulishwa vyema uwepo wake wanaweza wakagundua vingi vilivyomo
ambavyo vinaweza kuwa vivutio vya utalii.
“Mlima huu,bwawa lake,na uwanja mkubwa uliomo ndani
aliyefanywa watu wajue kuna nini.Ni marehemu Jua kali mwela ambaye kazi zake ni
kuwinda Nungunungu.Na kukuta maajabu ya ya uwanja mkubwa amabao unaweza
ukakusanya kijiji cha Mtonya”.
Ndani ya pango hilo kabla ya kuingia lazima upitie mbepesi kwenye
msola(mti) ambao unafagiliwa ili kumfanya Nyoka mkubwa anayeishi katika pango
ile aingie katika Chungu cha maajabu.Chungu ambacho mpaka leo hakuna
aliyethubutu kukisogelea na kujua kina nini zaidi.
Watu wanaofanya hivyo mara nyingi ni wale waganga ambao
hutumia maji haya mpaka kesho kuwatibu watu wenye mashetani na majini.
Maajabu yanayoweza kuleta tija ni uwepo wa eneo kubwa ambalo
ndani yake kuna wanyama kama Simba na chui wanaozaliana na kuishi humo.Bila
mnyama Nungunungu kuweza kuingia katika kitundu Jua kali asingeweza kugundua chochote.
ITAENDELEA ………..JUA SAFARI MPAKA MALIASILI NA YALIYOMO ZAIDI KATIKA MLIMA
CHAMANGA
0 maoni:
Chapisha Maoni