Na Hosea Mchopa #UO 1
Dunia imegawanyika vipande vipande kinachosubiriwa na kusagwa sagwa na kupoteza kila kilichomo.Hii ni hatari ambayo haiwezi kuzuilika kama ilivyo kwa kifo.Lakini umewahi kuwaza kuwa unaweza ukawa kijana mpaka kifo chako.Haijalishi utakufa na miaka mingapi.
Mimi
ninawaza sawa kama Henry Ford mmliki wa kampuni ya Ford Motor na mwandishi wa
kitabu cha My life and work kwa hili.Mtu yeyote anayeacha kujifunza huyu ni
mzee hata kama ana miaka 20 au 15.Na yule anayejifunza huyo ni kijana.Na siku
zote weka akilini kuwa u kijana na unaendelea kujifunza.
Katika
jamii niliyopo nageuka kulia na kushoto na kutana na vijana wanaopenda vitu
vilaini wakiamini wanahitaji akili ipoe kwa manufaa ya baadaye.Hawapendi
kujifunza,wanapenda kufanya wanavyohisi bila utafiti wowote uwe wa mahandishi
au sauti.
Ukiwa
kijana unakuwa unajiamini,wakati mzee huwa mwoga kwa kuwa u hafifu.Ukiwa kijana
unakuwa na matumaini wakati ukiwa mzee unakuwa hauna unachotumaini.Hii ndo siri
kwa nini vijana wengi Tanzania hawajiamini na hawana matumaini.Wao wamezeeka kwa
kuwa hawapendi kujifunza.
Kujifunza
ni zaidi ya kusikiliza radio na kuweka kichwani ni kutafiti zaidi,kuchambua
kitu kiundani.Leo hii hili ni kosa la jinai kwa kijana anayeishi kwa kujifunza
huonekana anajizeesha.Wao wanachukia uzee wakati kutojifunza ni uzee tosha.
Napata
shida sana moyoni nikisikia Taifa linategemea kitu kutoka kwetu eti tuje kuokoa
kizazi kijacho.Tumerahisishiwa ufaulu wa kidato cha nne,tunarahisishiwa ufaulu
katika vyuo vyetu tunapita kirahisi.
Tunapoteza
muda kuwaza kwa nini wazee wa zamani walikuwa na uwelewa mkubwa.Wao ilikupasa
uwe unafahamu kitu kiundani ndipo upate heshima katika jamii ya kitanzania.Sisi
leo hii cheti na makaratasi yaliyotengenezwa huleta uimara wa mtu kulikoni kile
alichonacho.
Henry
Ford aliyezaliwa mwaka 1863 mwezi julai 30 na kufariki april 7 mwaka 1947.Akiwa
na miaka 26 alikuwa tayari amesoma tafiti mbalimbali zilizomuwesha kuwa na afya
ya akili.Hii ilimpelekea kuwaza kutengeneza gari lake la kwanza likijulikana
kama quadricycle mwaka 1896.
Ili
uweze kuwaza kwa kina na kuvumbua mambo mapya hautajiki kuwa msikilizaji na
mpokeaji tu.Lazima upende kusoma kiundani ukitengeneza ndoto pevu zilijengeka
katika mbinu za kisomi na kuwa na mlango unaoshangaza.
Leo
hii vijana ni wepesi wa kusahahu hata ahadi walizoahidiwa na viongozi wao,miaka
mitano ikifika wakiahidiwa hushangilia tena.Akili zao zimezeeka kwa kuchukia
watu wanaobuni na kuwaza miaka miatano ijayo wakati wao kesho hawaijui.
Vijana
wanatumiwa na wazee katika upande wa siasa bila kujua huku wakilalamika bila
kukoma juu ya ugumu wa maisha.Akili zao hazina afya tena,wamekosa uwezo wa
kutafakari mambo kwa jicho la tatu.
Wamechukuliwa
na teknolojia upande hasi,si chanya kama inavyopaswa kutumiwa kusambaza hata
maneno ya mungu.Wao imewafanya washindwe kabisa kutembelea hata nyumba za
ibada.Hii ni siri kwa nini busara na unyenyekevu huishi mbali nao.
Mahatma
Gandhi Bapu mwanaharakati wa india huru alisema ishi kama utakufa kesho.jifunze kama utaishi milele.Asingejifunza
angeutumiaje ujana wake kuokoa jamii yake.Leo hii vijana ndio wanaotumiwa na
wanasiasa kuharibu maendeleo kuja kuwashangilia wanapoahadaa wananchi.
Elimu
si kujifunza dondoo na takwimu bali ni kukiweka kitu kichwani kukifuatilia na
kukitumia maishani.Kutoka hapo ulipo umefungwa na uvivu wa kujifunza,kukata tama
kunakotokana na kushindwa kujua wengine walifanyaje.
Wazee
wote wanaondelea kushangaza dunia walijifunza mengi katika muda wetu.Marie von
Ebner Eschenbach mwandishi wa Austria aliyezaliwa nchi ya jamhuri ya Czech na
mwandishi wa vitabu vya Their
Pavel, Beyond atonement alisema katika ujana tunajifunza kwa sababu ni
umri tunaoelewa.Usipotumia huu mda vyema utakuwa mzee mara mbili kimwili na
kiakili.
Vijana
wengi wa Tanzania ukitukuta katika makundi yetu tunasikistisha,tumekosa ubunifu
kabisa na akili zetu zimezidi kulala maradufu.Tunasema tuliyoambiwa bila ya
kuyatafiti,tukiulizwa tunaishia kuimba wimbo wetu alisema.
Bado
nipo chuoni najifunza na nawasoma vijana ambao hawajui hata fani yao wanaoisomea
nini kinaendeea katika serikali kuhusu wao.Vijana ambao watakuja kupiga kura ya
kumchagua rais wa Tanzania kwa kipimo cha anavyotangazwa katika vyombo vya
habari na sio sera zake.
Si
rahisi kuhisi umri umesogea kama akili yako inafanya kazi kama kijana.Umri ni
kuamua moyoni ila usipoamua uanabaki vilevile.Amini unaweza ukaishi milele
kijana ukiamua kutuamia ujana wako kujifunza.Ukiwa mzee wa mwili pekee utafurahi kufunua
kinywa ukiwa umezungukwa na vijana wengi wakichukua yaliyomo moyoni na
kujifunza.Jifunze zaidi uipeleke Tanzania mbali zaidi..Ujana ni kujifunza na
kubadilisha.
0 maoni:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.