Na Hosea Mchopa #UO 1

Huko nchini marekani JACKSONVILLE FLORIDA wanadoa Tito na Amanda Watts wamekamatwa na polisi kwa kosa la kuuza tiketi feki za dhahabu za kuwazesha watu kwenda mbinguni.


Baada ya kukamatwa Tito Watts akiongea kwa kujiamini alisema
‘’Sibabaishwi na walichokisema polisi.Hizi ni Tiketi za dhahabu halisi na sio kweli kuwa nimepulizia rangi.Ni Yesu mwenyewe ndiye alinipa pale nyuma ya mghahawa wa KFC huku akiniambia nikauze ili nipate fedha za kwenda anga ya juu’’Tito Witts alisema

‘’Kwanza nilikutana na kiumbe wa ajabu wa sayari nyingine anayeitwa Stevie ambaye aliniambia kuwa kama nikiwa na fedha ataninyakua mimi na mke wangu kwenye ungo wake unaopaa mpaka kwenye sayari yake amabayo imeumbwa kwa cocaine tupu.Nitaweza kuvuta unga wa cocaine kadri nipendavyo,tena bila malipo.’’

Tiketi ambazo iliwagharimu watu waliomini kutoa dola 99.99 ili kupata tiketi moja ya kuweza kufunguliwa lango la mbinguni.

Kosa kubwa ni kuwa Tito aliwaambia watu kuwa zilitengenezwa kwa dhahabu tupu na ukifika langoni mbinguni ukionyesha tu unaruhusiwa kupita.

Polisi wao wanakana na kusema wamemakamata kwa kosa la kulaghai kwa kudanganya ni dhahabu tupu wakati ni miti tu ambayo imepuliziwa rangi ya dhahabu.

Kwa upande wa polisi kuuza tiketi za kwenda mbinguni sio kosa ,kosa ni kulaghai watu juu ya tiketi za dhahabu tupu.

Tito akiongea kwa kujiamini alisema  wajaribu kumpeleka mtu asiye na hatia jela ndio watakiona cha mtema kuni.Kama ni kukamata basi akamatwe  YESU kwa sababu yeye ndio aliyenipa tiketi hizi na kuniambia nizue.

Na akahidi kuwa yuko tayari kumrekodi Yesu kwa kificho ili watu wanaombeza waamini juu anachosema
.
Watu hao wamekamatwa na jumla ya dola 10000,mabomba matano ya kuvutia unga na mamba mdogo

Kwa upande wa mke Amanda amesema nia yao ilikuwa kuondokana na dunia hii tuende zetu anga za juu tukavute unga wa cocaine.


‘Sijafanya chochote.Mume wangu ndio alikuwa  anauza hizo tiketi za dhahbu za kwenda mbinguni.Mimi nilikuwa muangaliaji’alisema Amanda
07 Apr 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top