Mwanamama Lacey Spears mwenye miaka 27 amefungwa jela miaka 20 kwa kosa la kumuua mwanae mwenye umri wa miaka 5 kwa chumvi.
Lacey mkazi wa Chestnut Ridge maili 32 huko Kaskazini mwa jiji la New York anatuhumiwa kumuua mtoto wake kwa kumuwekea chumvi katika vifaa maalumu vya kumlishia mtoto huyu aliyekuwa amelazwa hospitali.
![]() |
Lacey Spears akisikiliza hukumu yake |
Wakili mtetezi alipinga vikali hukumu hiyo huku akisema mteja wake Lacey hana hatia na kuilaumu hosptali iliyotaarifu kuwa mtoto huyu alikufa baada ya kuwekewa chumvi.
Jaji Roberto Neary wa mahakama ya White Plainis New York alimkosoa vikali mama huyo kwa tabia hisio ya kibinadamu ambayo amefanya kwa mwanawe ambaye amemzaa mwenyewe.
Lacey alijitetea kuwa baba wa mtoto huyo alifariki kwa ajali hivyo yeye kuhangaika kumpatia huduma ya ugonjwa yakiyomsumbua mtoto huyo Crohn' na Celiac yanaharibu utumbo mdogo na mmenge'enyo wa chakula.Hivyo mtoto huyo kupata maumivu makali ya tumbo.
0 maoni:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.