#news room
Rais wa UKRAINE Petro Poroshenko( mbele) akiondoka baada ya mazungumzo ya kusaka amani mashariki mwa Ukraine.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linataraji kukutana
kwa dharura leo Jumapili ili kuweka mikakati ya kuimarisha makubaliano ya
kusitisha mapigano Mashariki mwa Ukraine yaliyofikiwa mjini Minsk nchini
Belarus, wanadiplomasia wamesema.
Wajumbe 15 wa baraza hilo wanajiandaa kupitisha mapendekezo
yaliyoandaliwa na Urusi yanayotoa wito kwa pande zote kutekeleza makubaliano
hayo ambayo yanatoa makataa ya kusitisha vita kuanzia kesho Jumapili.
Makubaliano yaliyofikiwa na rais wa Urusi Vladimir Putin na viongozi
wa Ukraine , Ufaransa na Ujerumani, yameonekana kushindwa huku mapigano makali
ya siku Ijumaa yakisababisha vifo vya watu 28.
0 maoni:
Chapisha Maoni