Na hosea Mchopa
Ushindi wa goli 2 -0
walioupata Yanga dhidi BDF X1 ya Botswana umetoa taswira ya namana gani
klabu ya Yanga inahitaji kufanya mazoezi kwa juhudi zaidi ili kuweza kulinda
matokeo haya katika mechi ya marudiano.
BDF XI ya Botswana ambayo imeanzishwa mwaka 1978 yenye dimba
lake la SSKB inaweza kubadilisha matokeo hayo yakawa chungu kwa Tanzania kama
Yanga itajisahau kuwa mbinu pekee ndizo ziliwabeba kiurahisi na wala si kiwango
cha timu.
Mbinu walizotumia klabu ya Yanga za kupata goli mapema
dakika ya 1 kupitia kwa Hamis Tambwe ndizo zilisaidia kuwafanya BDF X1
mabingwa mara 7 wa ligi kuu ya Botswana
kucheza kwa kujihami zaidi na kutoa mwanaya kwa yanga kushambulia zaidi.
Kikosi cha BDF wakishangilia ubingwa wa ligi ya botswana
BDF X1 inaonekana haijakata tamaa na matokeo yaliyotokea Dar
es Salaam hivyo wanajipanga zaidi kwa kuwandaa vijana wake hatari kama
mshambuliaji Vincet Nzombe na Kabelo Seakanyeg kuja kubadilisha matokeo katika
mechi ya marudiano.
Baada ya Yanga kupata goli la pili kupitia kwa Tambwe dakika
ya 56 akipokea pasi kutoka kwa Ngasa Halfani.Kuanzia dakika ya 60 BDF
walibadilika na kuonyesha mashabiki uwezo wao mkubwa wa kutengenza mashambulizi
ya kushitukiza.
Kauli ya kocha wa BDF X1 Leetang Kgengwenyane imedhihirsha
wazi kuwa wao walikuja na mbinu ya kutaka sare zidi kwa kuwa walijua Dar es
Salaam watapata presha kubwa ya mashabiki hivyo aliwapongeza Yanga kwa
kuligundua hilo na kupata matokeo.
Sasa Letang anaijua Yanga anajua umuhimu wa Coutinho,Niyonzima
na Ngasa katika kutengeneza mashambulizi na anamfahamu Hamisi Tambwe kama ni
mtu hatari.Tusitarajie mteremko tena.
Kikosi cha Yanga kinahitajika kuifahamu vyema zaidi timu hii inapokuwa nyumbani pamoja na kupuza makosa yao baadhi ya wachezaji wake wanaopenda kukaa na mipira muda mrefu kama tulivyoona jana na tatzio la kujisahau kama alilofanya niyonzima na kunyang'anywa mpira na Kabelo ambaye almanusra alete matokeo mabaya kwa Yanga.
Soka la Botswana sio kubwa sana lakini tusitumie hiyo nafasi kuamini kuwa itakuwa rahsi kufanya tutakavyo nit timu ambayo inauchu ukizingatia mwaka 2004 ndio maraya mwisho kuchukua ligi ya nyumbani.Hatujua matamanio yao ni nini katika mashaindano hayo mwka huu.
Wanatamani wakifanye walichofanya mwaka 2002 walipofika hatua ya pili ya kombe la shirikisho kabla ya mwaka 2005 kumalizwa katika hatua ya kwanza.
0 maoni:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.