Na Hosea Mchopa
Christiano Ronaldo mfalme wa ureno katika ulimwengu wa soka anaendelea kusafiri katika ulimwengu mtamu wa maisha yake ya soka duniani.
Wakala wake Jorge Mendes alishawahi kuweka wazi kuwa Ronaldo hawezi kuhama klabu ya Real Madrid mpaka avunje rekodi muhimu za klabu hiyo na kutengeneza historia kubwa zaidi.
Mshindi huyo wa Ballon D'or ameanza kasi mpya kufukuzia rekodi ya mkali wa mabao wa klabu ya Real Madrid Raul Gonzalenz.
Jana katika mechi dhidi ya Elche alifanikiwa kufunga goli la 290 na kuifanya klabu ya Real Madrid kufika kileleni kwa tofauti ya point 4 dhidi ya Barcelona.
Sasa Ronaldo amefanikiwa kuwa juu ya mfungaji hatari wa zamani Carlos Santillana na kukamata nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote.
Ronaldo itamgharimu magoli 33 ili aweze kuvunja ufalme wa Raul Gonzalenz katika klabu ya Real Madrid.
Kwa upande wa timu ya taifa ya Ureno Ronaldo amekwamisha mipira 52 wavuni katika uwepo wake uwanjani akiwa na jezi la taifa mara 118.
Katika mchezo dhidi ya Elche hapo jana Karim Benzema aliianza kwa kufunga goli dakika ya 59 na Ronaldo kufunga la pili.
0 maoni:
Chapisha Maoni