Na Hosea Mchopa #UO 1

Kufikiri vyema kwa ajili ya baadaye kunahitaji kujitambua kuwa maisha yako ya leo yaliandaliwa na waliopita.Haupaswi hata dakika moja katika maisha yako kujifikiria wewe peke yako.Tafsri ya maisha yako itakuwa fupi sana u mbinafsi.

Sasa tujiulize utawekaje ubinafsi katika jambo ambalo linagusa zaidi ya watu milioni 40 tena litawaendesha kwa miaka 5.Hii ni safari ambayo bado watanzania wamejiandaa kukata tama kwa kuamini hawana uwezo wowote wa kuamua matokeo.

Si mbali ni karibu kuweza kuamini ukiwaza kwa ajili ya kizazi kijacho,ukiweza kuwaza hivyo unaweza ukagusa sehemu usiyoitarajia.Unafahamu hamasa unayopata ukipanga jambo jipya lenye kugusa maisha yako.Ndivyo amini unavyoweza kubadilisha malalamiko yako ya miaka mingi iliyopita.

Nakumbuka Agosti 28 mwaka 1963 katika kumbukumbu ya Lincoln,Washington DC Martin Luther alipoonyesha maana halisi ya binadamu anayetambua uwepo wake duniani.Aliweza kuwaonyesha watu kuwa kuwaza kwa kina kuhusu kesho kunaweza kukakufanya uamini kila kitu kinawezekana.
Martin Luther akihutubia tarehe 28 agosti 1963



Martin Luther aliamini vitu ambayo watanzania waliokuwa na mioyo iliyolala wasingeweza hata kuvumilia kumsikiliza.Sisi tunaishi na roho za bora hili kuliko lile lijalo,huku woga ukiwa katika kila sentesi itokayo vinywani mwetu.

Woga ni mbaya huharibu kabisa nafasi ya kitu halisi ambacho kinaamua mafanikio yako maishani.Chaguo ndio kitu muhimu katika mafanikio ya kitu chochote duniani.Kila kitu unachokichagua lazima kiwe na umuhimu kwa kizazi kilichopo na baadaye.

Usiogope kuwaza kuwa unataka kuiona Tanzania inayoongoza kwa elimu  katika umoja wa jumuiya wa nchi za Afika Mashariki baada ya miaka 5.Chaguo lako ndio litachagua mwelekeo wako wa nini unastahili kutokana na ulichokiwaza kiwe.Hutakiwi kabisa kuficha maono yako nyuma ya pazia na kutanguliza roho ya woga kuwa mabadiliko katika ardhi yetu hupangwa na watu wenye nguvu.

Tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa wa nchi ya Tanzania ambayo ina sifa ya amani na upendo.Lakini wote tuishio tunajua nini kipo katika ardhi hii,tunafahamu mambo ya kushangaza ambayo yanazaliwa na kuachiwa bila hatua kuchukuliwa.

2015 ni wakati wa kuwaza katika maono ya mbali na kuweka woga wetu pembeni ambao umeingia katika roho zetu.Woga ninaongelea ni ule wa kuamini mimi siwezi kubadili Tanzania kwa kura yangu,kwa mawazo yangu,kwa uwepo wangu katika sehemu yoyote ile.

Woga hupelekea mtu kushindwa kutafsri vyema mambo yatakiwavyo kuwa.Woga humfanya mtu kushindwa kutofautisha vitu vidogo ambavyo yeye anahitajika kuvipata.Humfanya mtu kuamini hawezi kuileta A kama aliye juu anapenda B.

Lazima ujue Tanzania ya leo na ijayo watu wanahitaji Kiongozi ambaye anaishi kwa tafsri halisi ya uongozi.Mtu ambaye yupo katika nafsi ya urais,ubunge  kufanya majukumu ambayo kiongozi wa nafasi hiyo anapaswa kufanya akifuata sheria na kanuni zilizowekwa ili aweze kuongoza kundi kubwa la watanzania.

Tutofautishe kabisa na madikteta ambao wanasimama katika nafasi ya urais kama makocha wanaotaka kila kitu ambacho wao wanachopendaa timu ikifanye.Wale ambao hawahitaji michango zaidi ya kuelekeza watu wafanye wao wanavyopenda bila kufuata kanuni.Na wanafanya hayo yote kwa kauli kuu kuwa wa ndio wenye mamlaka.

Woga utamfanya mwanao ajae akute serikali iliyokosa uwazi kwa kuwa uliuendekeza ukashindwa kuamua chaguo sahihi.Ukashindwa kumchagua kiongozi ambaye anafanya kitu inavyopaswa hata kama hakuna mtu anayemtazama na kumsifu.

Kama utaweka woga mbele utashangaa kuona kiongozi sahihi akiwaza kuiona Tanzania ikiwa ina umeme na maji vijijini.Hivyo utaishia kuiletea Tanzania kiongozi mwenye maono na kuifanya familia yetu ibakie vilevile kimaendeleo.Na siku zote kiongozi asiye na maono huwa hajitambui kuwa yupo katika uongozi kama wajibu tu anapaswa aache alama akitoka.

Tunahitaji kusikilizwa watanzania kwani kuna vitu vingi vitahitaji marekebisho ambayo yataleta faida katika nchi yetu.Tutampata wapi kiongozi anayetusikiliza kama woga wako umekupeleka kushindwa kumtofautisha kiongozi anayekujali wakati wa kampeni na kiongozi ambaye anajali shida za watanzania?.

Kiongozi ambaye atakuwa ana uwezo wa kusoma alama za nyakati na kutoogopa kufanya maamuzi ambayo yanaweza hata yakamuumiza yeye kwa ajili ya usalama wa watanzania.

Martin Luther aliamini maisha watoto wake siku moja watakuja kuishi katika taifa la Marekani ambalo hawataishi kwa kuangaliwa rangi zao za ngozi kama ilivyokuwa wakati huo.Aliacha woga akamini pamoja na wabaguzi wana nguvu lakini jamii ikiamua kutaka kilicho bora inawezekana.


Jenga daraja jipya kuelekea 2015 katika moyo wako ukiishi kwa maono na kutumia nafasi ya chaguo vyema kwa ajili ya Taifa.Ishi kwa ndoto!.
24 Feb 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top