Mchezaji haruhusiwi kwenda mjini kujiburudisha masaa 48 kabla ya mchezo.Hii ndio ilikuwa kanuni ya kocha wa zamani wa Mancheser City Robert Mancini.Na Mario Balotelli aliwahi kuadhibiwa kutokana kukiuka kanuni hii.
#hii kwa ajili yako
Inawezekana kukawa na hali inayoashiria Luis Enrique na
Lionel Messi bado hawajawa katika muungano unaohitajika.
Leo asubuhi ikiwa ni
masaa 48 kabla ya kuelekea katika mchezo mkali wa ligi ya mabingwa ulaya kati
ya Barcelona wakialikwa na Manchester City katika dimba la Etihad.
Lionel Messi,Gerard Pique na Cesc Fabregas mchezaji wa
Chelesea walikuwa wakijumuika pamoja katika Casino .
![]() |
Lionel Messi,Fabregas na Luis Enrique wakiwa nje ya Casino |
Akizungumza Katika mkutano na wahandishi wa habari za
michezo kuelekea mchezo wa UEFA.Kocha Enrique ameonesha wazi kutohitaji
kulizungumzia suala hilo kwa sasa.
Ni maisha yangu binafsi.Ni kauli ya Gerard Pique akijibu
kashfa ya kwenda kwenye Casino masaa 48 kablya ya mechi.Huku kocha wake
Enrique akihitaji kutoulizwa maswali yasiyohusu mpira wa miguu na hatovutiwa
kuyajibu yale yaliyo nje ya kazi yake.
Uhusiano mbovu kati ya kocha Jose Enrique na Lionel Messi
yalipamba moto pale kocha alipoamua kumweka benchi Messi wakati timu yake ikipewa
kichapo cha goli1-0 na Real Sociedad.
![]() |
Gerard Pique na Lionel Messi wakiwa mazoezini |
Bado Enrique ameweka wazi kuwa mahusiano na wachezaji wake
yako sawa na anapenda kuongelea na kuchambua kuhusu vitu vinavyohusu mpira wa
miguu na sio maisha binafsi.
Lakini jamii na familia ya soka tunamtambua na kumfahamu
Enrique kuwa ni baba wa nidhamu.Na ni kitendo kisichopenedeza kwenda klabu
masaa 48 kwenda klabu kabla ya mchezo.Je ataamua nini siku za usoni.
![]() |
Kocha wa klabu ya Barcelona Luis Enrique akizungumza na wahandishi wa habari hii leo |
Enrique alipotua
Stadio Olimpico Roma alifanya maajbu makubwa sana ya kupambana na wafalme
waliotengenezwa miaka mingi katika klabu hiyo.Daniel De Rossi pamoja na
Fransico Totti walipambana na roho ya udikteta wa nidhamu wa Enrique.
Hakuweza
kuvumilia kuona Danie De rossi anachelewa katika mechi ya maandalizi kwa sababu
ni mkongwe wa timu.Hakuwa na mashaka kumwacha nje nahodha wa timu Totti baada
ya kuvunja sheria zake za kutofanya mazoezi ipasavyo kabla ya mechi.
0 maoni:
Chapisha Maoni