Na Hosea Mchopa #UO 1

Ni dhahabu nyeusi kutoka Lagny sur Marne “Polpo Paul II’ au Patric Viera mpya.Wataalamu wa soka wanamtambua kwa vielelezo vitatu nguvu,ujuzi na ubunifu.

Ukiwa Italia ukiperuzi kona zote za michezo La Repubblica ,II Messaggero na La Gazzeta Dello Sport lazima ukutane na sura yake.Kocha Alex Ferguson kila mara hukubali kumwacha binadamu huyu alifanya makosa makubwa sana.

Mchezaji wa kimataifa wa Hispania na Manchester united Juan Mata anakata tamaa kila akiona jina la Polpo Paul II limeambatanishwa na Manchester united.Anajua hivi sasa ukizungumzia katikati mwa uwanja katika ulimwengu wa soka unamtaja yeye.Mata anajua kibarua kimeota nyasi.

Dhahabu nyeusi Paul Labile Pogba ‘Polpo Paul II’ mwenye kilo 80 ndiye anayetishia dunia ya soka hivi sasa.Sekunde,dakika na masaa yanavyozidi kwenda akiwa katikati ya uwanja ndivyo thamani ya pesa yake inavyoongezeka kwa kasi kwa vitu anavyovifanya.
Paul Pogba


Akiwa bado kijana mdogo mwenye umri wa miaka 21 amefanya kila kitu ambacho mchezaji kamili anatakiwa akifanye.Ama hakika amekamilika kiuchezaji,miguu mirefu na mwili imara humtambulisha yeye ni nani.

Ukiitazama miguu yake itakupa somo kuwa yuko tayri kukimbizana nawe na kukunyang’anya mpira vile apendavyo.Patric Viera mpya anayemezewa mate na vilabu vikubwa barani ulaya.

Mkongwe wa Italia na Juventus  Andre Pirlo amemtaka aachne na fikra za kuhamia igi kuu ya uingereza na kuamishia akili zote Juventus.Lakini kwa hali hii ya kawaida nani ataweza kumzuia Pogba asiondoke Juventus.

Miaka 21 kila umri unaposogea ndivyo anavyozidi kuimarika na kumfanya kocha mwenye matukio Jose Mourinho kukuna kichwa akimtazama Abramovich.Ni kama mvinyo siku zinavyozidi ndivyo huwa mtamu zaidi.

Mkongwe wa ufaransa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea takribani miaka 4 Nicolas Anelka anahitaji kumuona Paul Pogba anajiunga na klabu ya Chelsea anakuwa katika mikono ya tajiri Roman Abramovich.

Anelka anahitaji kumuona anaenda Real Madrid katika klabu kubwa duniani akajifunze mengi kutoka kwa kocha mwenye rekodi ya kipekee kuchukua UEFA akiwa na AC Milan na Real Madrid Carlo Anceloti.

Pogba mzaliwa wa Lagn sur Mane ufaransa alitwaa mchezaji bora chini ya miaka 21 barani ulaya katika tuzo za Golden Boy mwaka 2013.2014 akatangazwa kama mchezaji bora barani ulaya chini ya miaka 23 katika tuzo za Bravo.
Mchezaji wa Juventus Paul Pogba akishangilia goli


Mwaka 2014 ulikuwa wa kipekee kwake katika kombe la dunia aliweza kufunga bao kwa timu ya taifa brazili tarehe 30 juni 2014.Katika mechi dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.Kutokana na kiwango alichoonesha katika kombe la dunia 2014 akachaguliwa kuwa mchezaji bora mdogo wa dunia.

Kiungo mkabaji na kiungo wa kati ni majukumu ambayo ukimpa hautajutia uamuzi wako kabisa. Ni roho ya Juventus ana jeuri ya kufikisha  mipira atakako,ana uwezo wa kufika kila kona ya uwanja.

Mechi 19 za Seria A amefunga mabao 6 na kutengeneza goli 2 katika dakika 1700 tu alizocheza.Dakika 537 kwa upande wa ligi ya mabingwa ulaya ameona nyavu mara 1 na pasi 1iliyozaa goli

Ana uwezo mmkubwa wa kunyang’anya mipira na kupiga pasi ndefu zianzofikia wahusika.Msimu huu ana wastani wa silimia 83 wa kupiga pasi sahihi.Kazi ziliwashinda viungo wengi waliopo kwa bahati kalbu kubwa.

Hakuna taarifa inayovutia wapnzi wa soka kama taarifa ya Louis Van Gaal kusema anahitaji kiungo mbunifu zaidi katika dirisha la usajili lijalo.Sasa Wayne Rooey Pekee ndio anaweza kukabili majukumu hayo United.Hili ni fumbo tu lakini Van Gaal anamuhitaji Pogba.

 Macho ya vyombo vya habari hayana mashaka kabisa juu ya mapungufu yaliyopo Manchester united yanahusiana kabisa na uhitaji wa kiungo hatari kama Pogba.Je ? ni nani hasa atajiunga na Manchester United,hatupaswi kusahau kuhusu IIkay Gundogan ambaye ananukia kinywani mwa Van Gaal.
Paul Pogba akiwa katika jezi la Manchester united

           
19 Feb 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top