Bado taarifa za mtoto wa aliyekuwa msanii maarufu na hodari
wa mziki wa RnB duniani Whitney Houston ambaye tayari amefariki duniani.
Bobbi Kristina Brown zinazidi kushika ulimwengu wa vyombo
vya habari duniani huku ikiripotiwa baadhi ya viungo vya mwili vimeshindwa
kufanya kazi kabisa na kutumia vifaa maalumu kusaidia uhai wake usipotee.
Mpya mpenzi wa Binti
huyo Nick Gordon ameonekana
kushindwa kabisa kupoteza mawazo juu ya mpenzi wake na kujaribu zaidi kuomba
nafasi ya kumuona alikolazwa.
Tangu januari 31
baada ya taarifa kuenea juu ya Bobbi Kristina,Gordon hajaruhusiwa na Familia
kuweza kumuona mpezni wake.
Mwanasheria wake wa Atlanta Randly Kessler amesema ‘ Nick amejaribu,binafsi,kufanya kila
kinachowezakana kumuona Bobbi Kristina’.Anachotaka Nick ni kumuona binadamu
anayempenda Bobbi na anatumaini ombi lake litafanikiwa.
Inataarifiwa kuwa jeshi
la Polisi Rosweell huko Marekani
limefungua uchunguzi wa uhalifu wa kesi hiyo na Gordon ni mmoja ya watu
watakaohusika kufanyiwa uchunguzi kujua chanzo cha yaliyomkuta Bobbi Kristina
Gordon anaingizwa katika shutuma hizo kutokana na mwili wa Bobbi Kristina Brown umekutwa una
majeraha na kuhisiwa Gordon anahusika juu ya hilo.
0 maoni:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.