Fc Basel ikiwa nyumbani St Jakob Park kuikaribisha Fc Porto
katika usiku wa mabingwa ulaya mambo ya kuvutia yalijitokeza katika mechi hiyo
ngumu ambayo iliisha kwa sare ya goli 1-1.
Kocha wa Fc Porto Julen Lopetegui na kocha wa Basel Paulo Sousa
Mwamuzi Mark Clattenburg ambaye
msimu uliopita alikosolewa vikali na kocha wa Juventus ,aliongoza mechi kali na
ya kipekee mbele ya mashabiki 34,464 waliokata tiketi
kutazama mechi hiyo.
Dakika ya 11 tu iliwapa raha mashabiki wa Fc Basel baada ya mchezaji
wa kimataifa wa Paruguay Derlis Gonzalez kufunga bao na kuwapa matumaini Fc Basel
katika mchezo huo.
Gonzalez wa Basel akifunga goli dakika ya 11
Clattenburg pamoja na kukata goli la Porto dakika ya 79
aliwazawadia penalty Porto na Danilo kukwamisha wavuni na kufanya matokeo
yaishe kwa goli 1-1.
Danilo akifunga goli kwa njia ya penati
MAMBO YA KUVUTIA
Katika mechi ya jana mwamuzi Mark Clattenburg alitoa kadi 9 za
njano.kadi 5 kwa Basel na 4 kwa Porto.
Mwamuzi Clettenburg akimuonesha kadi ya njano mshambuliaji wa Porto Torres
Kadi hizi zimeweka rekodi na kuifanya kuwa mechi peke kuwa na kadi
nyingi kwa masimu huu.
Fc Basel hawajawahi kuingia katika hatua ya robo fainali ya mashindano
ya ulaya tangu msimu wa mwaka 1973-74.
Jana Danilo alikuwa ni mchezaji wa tatu wa Porto kufunga kwa njia
ya penati msimu huu baada ya Ricardo Quaresma na Jackson Martnez kufanya hivyo.
Mchezaji wa klabu ya Porto Danilo
#UO TUNAAHIDI KUKUPA KILE UNACHOSTAHILI
0 maoni:
Chapisha Maoni