Na hosea Mchopa #UO 1

Usiku wa mabingwa ulaya ulizidi kushamiri kwa kuleta mambo ya kuvutia na rekodi za kipekee katika usiku wa jana pale mabingwa Real Madrid walipokaribishwa na Schalke 04.



Pamoja na kumbukumbu mbaya za Schalke  kutolewa na Madrid katika hatua kama hii kwa jumla ya goli 9-2.Jana wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki 54,442 walijitahidi kupambana vilivyo kuweza kuwazuia Madrid wasifanye maajabu zaidi.

Ilimchukua dakika 26  mwamuzi Martin Atknson kupuliza kipyenga cha goli baada ya mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo kumaliza ukame wa mabao baada ya kutoona wavu kwa mechi tatu zilizopita.Alikuwa ni Dan Carvjal ndiye aliyetengeneza mpira mzuri na Ronaldo akiumaliza kwa kichwa.

Kama haitoshi Ronaldo jana akageuza usiku wa mbingwa ulaya kuwa wake baada ya kutengenza goli la pili kwa Marcelo ambaye aliweka kimiani goli dakika ya 79.

MAMBO YA KIPEKEE KATIKA MECHI YA SCHALKE NA REAL MADRID.
Timu ya Schalke haijawahi kushinda kombe la mabingwa ulaya lakini kocha wake pekee Roberto Di Matteo amewahi kulibeba kombe hilo akiwa katika klabu ya Chelsea.
Kocha wa Schalke Di Matteo


Beki raia wa Brazil Marcelo goli lake la pili jana dakika ya 79 ndio goli lake la pili kwa msimu huu.
Marcelo akishangilia goli lake alilopachika dakika ya 79

Cristino Ronaldo Jana amefanya maajabu ya aina yake kwa kufunga magoli 58 katika michezo 58 ya ligi ya mabingwa ulaya.
Mshambuliaji wa Real Madrid Ronaldo akishangilia goli lake la 58

Klabu ya Real Madrid imeitambia Bayern Munich baada ya kushinda michezo 10 mfululizo bila kufungwa.

Vikosi vya jana
Schalke 04
·         40 Wellenreuther
·         22 Uchida
·         04 Höwedes
·         32 Matip
·         31 Nastasic
·         15 Aogo
·         12 Höger (Meyer - 80' )
·         33 Neustädter  (Kirchhoff - 57' Booked )
·         09 Boateng 
·         25 Huntelaar (Platte - 33' )

·         13 Choupo-Moting


Real Madrid
·         01 Casillas
·         15 Carvajal (Arbeloa - 82' )
·         03 Pepe
·         02 Varane
·         12 Marcelo
·         16 Borges
·         08 Kroos
·         23 Isco (Illarramendi - 85' )
·         11 Bale
·         09 Benzema (Hernández - 78' )
·         07 Ronaldo



0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top