Na Hosea Mchopa #UO 1

Unapenda kutazama  filamu ambazo zinanguvu kubwa katika ulimwengu wa filamu katika mwaka 2015.Kama wewe ni mpenzi  wa kuenda na wakati katika upande wa filamu basi taarifa hii ni kwa ajili yako.

Mwaka 2015 ulivyoingia wakongwe mbalimbali walijitahidi kutaka kuanza vizuri katika mwaka huu ili wapate kujiamini zaidi katika ulingo huu wenye ushindani zaidi.

Mpaka kufikia mwezi februari tarehe 20 hizi ni filamu ambazo zinatikisa ulimwengu wa filamu duniani na ukiwa mmoja wapo utakayetazama basi utakuwa bado hujaachwa nyuma kabisa.

1.NATION GALLERY
Ni filamu iliyotengenezwa katika mtindo wa makala katika jumba la makumbusho.Imeongozwa na muongozaji mahiri Fredric Wiseman.Ikiwa na urefu wa dakika 180 kuweza kufahamu kiundani elimu na mambo ya kisayansi yaliyomo.Frediric Wiseman na Pierre Oliver Bardet ndio walioandaa kazi hii.


2.SEVENTH SON
Ingizo jipya la februari 2 mwka 2015 ikihitaji dakika 120 kuweza kumtazama Master Gregory (Jeff Bridges) katika Seventh Son.Sergei Bordov amesimamia kazi nzima akishirikiana na wahariri Michael Khan na Paul Rubbel.

Waigizaji vinara
Jeff Bridges
Julianne Moore
Ben Branes

3.THE HOMES MAN
Muongozaji Tomm lee Jones ilimpasa kufanya kazi zote mbili kuongoza kazi hi pia kuigiza katika waigizaji vinara wa The homesman.Ni simulizi nzuri iliyoandikwa na Glendon Swarthout na kuandikiwa muongozo na vichwa vitatu.Wesley Oliver,Miles Hood,Kieran Fitzegerald.

Waigizaji vinara
Tom lee Jones
Hilary Swank
Meryy Steep

4.A MOST VIOLENT YEAR
Simulizi ya J.C Chandor inayomuhusu Oscar Isaac katika miaka ya 1981 ni moja ya filamu bora zinazoendelea kutazamwa.Itakupasa kukaa katika kochi lako dakika 125 kuweza kuona kazi iliyoongozwa na J.C Chandor.

Waigizaji Vinara
Jessica Chastain
Oscar Isaac
David Oyeolowo.

5.BIG EYES
Tim Burton ameongoza dakika 106 za filamu ya Big Eyes  ambayo inasimulia kisa cha miaka ya 1950 na mwanzo mwa miaka ya 1960.Scot Alexander na Lary Karaswezski wametengenza muongozo mzuri uliopanga matukio ya filamu hii.

Waigizaji vinara
Amy Adams
Cristoph Waltz
Krysten Ritter


6.ROSEWATER
Katika filamu hii nje ya mahudhui mazuri na ubora wa picha ambao unavutia kutazama.Kitu kikubwa unachopaswa kufahamu Muoongozaji John Sewart ndie aliyeandika mwongozo peke yake katika filamu hii ya Rosewater.Itakuchukua dakika 103 kuweza kutazama simulizi tamu iliyoandikwa na Aimer Mollay na Mazia Bahar.Ina mzungumzi mwadishi wa habari Maziar Bahar.



7.TERMINATOR GENIYS
Filamu kali sana yenye utumiaji wa teknolojia ambayo imetoka mwaka 2015.Kampuni ya uzalishaji ya Skydance ndio imeandaa hii kazi ya kipekee.Alan Tayrol amefanya kazi kubwa ya kuongoza fialmu hii.Kwenye upande wa muongozo wa filamu,Laeta Kalogrids,James Cameroon,Patric Lussier wameshirikiana pamoja kupanga matukio yasiyochosha.

Waigizaji vinara.
Arnold Schwarzeniger
Emilia Clark
Douglas Smith

8.71.
Filamu kali ya mapambano ambayo ianmzungumzia kijana Jack O’Connel .Muungozaji wa Fialmu hii ni Yann Demmange huku mwongozo ukiandikwa na Gregory Burke.Tayari filamu hii inatunzo ya British independent film kwa upande wa muungozaji bora.Na inaurefu wa dakika 100
Waigizaji vinara.
Jack O ‘Connel
Sean Harris
Sam Reid.


20 Feb 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top