Na Hosea Mchopa #UO 1

Ushindi wa jana wa Juventus dhidi ya Dortmund umewafanya wafikishe mechi 47 bila kufungwa wakiwa katika uwanja wa nyumbani.


#hii kwa ajili yako
Pamoja na klabu ya Borussia Dortmund kutawala mchezo kwa asilimia 53 kwa 41 za Juventus walikubali kichapo cha goli 2-1.

Kinara wa magoli wa Juventus Carlos Tevez alitumia dakika 13 tu kuweza kumgalagaza kipa wa Dortmund Weidenfeller.

Marco Reus kiungo anayevutia barani ulaya kwa sasa alimtungua mkongwe wa Italia kipa Buffon dakika ya 18 tu na kurejesha hali ya ushindi Dortmund

Alvaro Morata akafunga bao la pili kwa Juventus dakika tatu kabla ya kipindi cha kwanza kuisha na kufanya wenyeji watoke kifua mbele kwa jumla ya goli 2-1.



Kocha wa klabu ya Dortmund Jurgen Klop moja kwa moja ameyakubali matokeo hayo kuwa yalikuwa ya haki na kuwapongeza Juventus kwa kuweza kutumia vyema nafasi mbili kubwa walizopata.


Mechi za leo
Wednesday, February 25
Arsenal vs Monaco
10:45 PM

Bayer vs Atletico Madrid
10:45 PM


25 Feb 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top