Na Hosea Mchopa

Mechi hii inaifanya klabu inayotetea kombe la ligi kuu uingereza Manchester City kutofanikiwa kabisa kupata ushindi  katika uwanja wa nyumbani wa klabu ya Liverpool Anfield tangu may 2003.


#hii kwa ajili yako
Mbele ya mashabiki 44,590 mwamuzi mahiri katika ligi kuu ya Uingereza Mark Clatternburg alilazmika kupiga kipyenga cha goli dakika ya 11 tu ya mchezo huo baada ya Henderson kufunga bao.


Goli la Henderson lilisawazishwa  katika kipindi cha kwanza tu cha mchezo huo baada ya Edin Dzeko kuwasimamisha mashabiki wa city kwa bao lake tamu dakika ya 25.

Mchezaji wa kimataifa raia wa Brazil Phippe Coutinho ameiwezesha klabu yake y a Liverpool kuweza kusogea hadi nafasi ya tano pointi 2 nyuma ya Manchester United.

Matokeo ya Leo yanaifanya klabu ya Chelsea kuizidi klabu ya Manchester City kwa jumla ya point 5.

MUHIMU KUFAHAMU

Goli la kwanza la Henderson la ligi kuu ya uingereza alilifunga dhidi ya Manchester city akiwa na Sunderland na jana alifungia Liverpool goli la kwanza katika ushindi wa bao 2.


Liverpool wamejitengenezea rekodi ya aina yake kwa mwaka wa 2015 kutofungwa katika ligi kuu ya uingereza.

Vincet company alifanikiwa kufikisha mechi 200 za ligi kuu uingereza.

Mfungaji wa bao pekee la Man City Edin Dzeko amwefunga mabao manne msimu huu.


Kocha Brendan Rogers alijitengenezea rekodi nyingine dhidi ya Manuel Pellegrini kwa kushinda mechi mbii na kupoteza mbili.

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top