Na Hosea Mchopa
MICHEZO YA FA
YALIYOJIRI DIMBANI NA MECHI ZA LEO

Derby Counry 2-1 Reading
Mbele ya mwamuzi  craig Pawson  mashabiki 21337 waliongia uwanjani walishuhudia Derby County ikifunga Reading kwa goli 2-1.
Magoli ya Derby yalifungwa na Robson Kanu dakika ya 53 na mchezaji aliyetoka bench Yakubu Aiyegbeni daika ya 82.
Mshambuliaji wa ReadingDarren Bent

Mchezaji hatari wa Reading Darren Bent alifunga goli lake moja dakika ya 61.Huku mchezaji wao Warnok akipewa kadi nyekundu
Crystal Palace 1-2 Liverpool
Mchezaji aliyerejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi ,mshambuliaji Daniel Sturridge ameisaidia timu yake kuizamisha klabu ya Crystal Palace kwa goli 2-1.
Sturridge mwenye miaka 25 alifunga bao lake dakika ya 49 na Adam Lallana akifunga la ushindi dakika ya 58.
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge akifunga goli

Kwa upande wa Palace Campell alipatia bao dakika ya 15

Liverpool wameshinda mechi 4 kati ya 5 ambazo Surridge amecheza tangu arejee dimbani na ushindi wa jana unawapeleka hatua ya robo fainali ya FA.

Morrison alifunga bao la pili dakika ya 42.Kabla ya Mshambuliaji hatari Berahinho kufunga bao la mwisho dakika ya 72

West Brom 4-0 West Ham
Mbele ya refa Martin Atson mchezaji hatari wa klabu hiyo Brown Ideye alifunga mabao mawili katika dakika ya 20 na 52.
Mchezaji wa West Brom Brown Ideye aipachika bao

Klabu ya West Brom imetinga hatua ya robo fainali toka mwaka 2008 baada ya kuifunga West Ham kwa jumla ya goli 4-0
Wachezaji wa West Brom Said Berahinho na Gadner  wakifurahi ushindi 


Blackburn 4 – Stoke 1
Joshua King amefanikiwa kufunga magoli matatu 'hat trick' na kuiwezesha kalbu yake ya Blackburn kuizamisha  Stoke City kwa jumla ya magoli 4-1.
Peter Crouch wa stoke city alikuwa wa kwanza kuziona nyavu katika dakika ya 10 ya mchezo na kutoa mwanga wa klabu yake.
Mchezaji wa Blackburn Joshua King akiisawazishia goli tim yake


King alifanya mauaji makubwa dakika ya 36,50 na 55 na kufanikiwa kuondoka na mpira baada ya mchezo kuisha.
Mshambuliaji Gestede alifungia goli Blackburn kwa njia ya penati dakika ya 45

mechi za leo
Astoni Villa  v Leicester
Bradford  v  Sunderland
Arsenal  v Middlesbrough
15 Feb 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top