Na hosea Mchopa
Omdurman mmoja ya miji yenye joto kali kabisa duniani kuna
wakati hufikia kiwango cha joto nyuzi 53
c na hali ya kawaida huwa 37 c.Ni mji mkubwa katika nchi ya Sudani ni kiungo
cha biashara ,kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2008 kuna wakazi karibu
2,395,159.Wachezaji kumi na moja wa Azam watapambana na sura za msahabiki 43655
katika mji huu.
Klabu ya Azam ya Tanzania yenye makao yake Chamanzi ina
kibarua kikubwa sana cha kuendeleza machungu ya klabu ya Al-Merreikh almaarufu
mashetani wekundu wa Sudani.Mbele ya Mashabiki 43655 katika dimba la nyumbani
la Al – Merreikh.Ni nani John Boco
atakayetibua kibarua cha Mjerumani mwenye roho ngumu kocha Michael Krugel.Si
timu ya kubeza 15 mwezi 1 mwaka huu waliamua kupimana ubavu kirafiki na timu kali
ya ujerumani ya Schalke 04 na kutoka sare ya goli 2-2.
Sina shaka bado tunakumbuka vyema furaha ya ushindi
tuliopata katika jiji letu la Dar es Salaam lakini ninaona jitihada zaidi
inahitajika kutikisa mji wa Omdurmani.Tarehe 27 mwezi wa 2 tutajua nani
atakutana na Lydia Ludic ya Burundi au Kabuscrop do Palanca ya Angola.
Mechi iliyopita tumlishuhudia mshambuliaji wa Azam John
Bocco akiendeleza uwezo wake mkubwa wa kufunga magoli muhimu kwa klabu ya
azam.John Bocco alichukua nafasi ya Kipre Tcheche dakika ya 77 na dakika ya 78
akafunga goli ikiwa ni mpira wake wa kwanza tu kugusa.
Jamii ikakumbuka uwezo wake huu wa kufunga magoli muhimu ya
Azam mwaka 2008 alifunga goli lililoipandisha timu yake ligi kuu.Aliswazisha
dhidi ya yanga katika mechi iliyoisha kwa goli 2-2 desemba 28 mwaka 2014.
Timu kongwe ya Sudan Al –merreikh inaongoza ligi kwa
kushinda michezo mitatu na kutoa sare mchezo mmoja kati ya michezo minnne.Timu
pinzani ya Al hilal inakamata nafasi ya pili ikiwa imeweka kibindoni pointi 8Kabla
ya kuumana kwa mara ya pili na klabu ya Azam itakutana na Merreikh El-Fasher ambayo inashika nafasi ya sita.Mechi hii itakuwa
ni darasa ndogo kwao katika kuivaa Azam Fc.
Kuna mambo mmengi wanakosa na wanahitaji kuyafanya ili kuweza
kupambana vizuri na Azam FC.Hasa katika
eneo la ulinzi wanaonekana na wanaudhaifu wa kutegeana.Na hii lipelekea kocha
kumuingiza Mohamedi Traore ili apunguze makosa katika mechi ya Chamanzi.
Uwepo wa Pascal Wawa raia wa Ivory Coast pia ni tatizo kwa
ngome ya Azam kupenyeka kirahisi kwani anaiujua vyema klabu yake ya zamani.Nafikiri
mwalimu Omong amejifunza mengi kupitia Wawa kutokana na uzoefu aliokuwa nao.
Mwaka 2014 katika ulimwengu wa mabingwa Afrika hawakuwa
vizuri baada ya Kampala city Council ya Uganda kuwafungisha virago Al-Merreihk
katika mzunguko wa kwanza.Waliwafungwa 2-0 na walipokanyaga kwao wakashinda
2-1,Lakini hakusaidia kuwatoa.
Recreativo do Libolo nayo iliwakatisha tamaa mzunguko wa
pili tu mwaka 2013 kwa kipigo cha 2-1 na marudio 2-1.Mwaka 2012 alikuwa
mtanzania Mbwana Samata alishiriki katika kuwaondoa katika ushindi wa TP Mazembe goli 2-0 kabla ya kutoa sare ya
goli 1-1 Katika Rundi ya tatu.
‘The leader’ wa Sudan
hawana cha kupoteza katika kombe la mwaka huu wanahitaji mafanikio zaidi katika
kombe hili.Kwenye Kabati Omdurman
wanavikombe 19 vya ligi kuu ya sudani na vikombe 24 vya kombe la
ligi.Wanahitaji historia zaid huku .Mjerumani Michael Krugel anahitaji
kutengeneza dunia ya kipekee Sudan hataweza kama Kavumbaga na John Bocco watang’ara Sudan
0 maoni:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.