Na Hosea Mchopa #UO2
Nimetoka katika klabu kubwa kwenda klabu kubwa .Ni nafasi ya nzuri kwangu.
Kauli ya Sherwood
Tim Sherwood amechaguliwa kuziba nafasi ya kocha
aliyefungishwa virago Paul Lambert baada
ya kutofanya mambo ambayo klabu ya Aston Villa yalitegemea.
Tim Sherewood mwenye miaka 46 ameonekana kuikubali kazihiyo
kirahisi mara baada ya kupigiwa simu na siku ya jumamosi alikuwepo kuishuhudia
Aston Villa ikimuadhibu Leicer City goli 2-1.
Wachezaji wa Aston Villa wakishangilia ushindi dhidi ya Leicer City
Majukumu ya mwanzoni ya kocha huyu ni kumrejesha mchezaji
ambaye Arsenal Wenger alihitaji hudumu yake msimu uliopita Christian
Benteke.Benteke ndiye alikuwa roho wa Aston Villa hivi sasa amefinga bao 3 tu katika
mechi 19.Katika misimu miwili iliyopita alifunga mabao 34 katika mechi 64.
Mshambualiaji wa Aston Villa Christian Benteke
Timothy Alan Tim Sherwood
alizaliwa February 6 mwaka 1969 .Alikuwa mchezaji katika nafasi ya
kiungo toka mwaka 1987 hadi alipostaafu 2005.
Kocha mpya wa Aston Villa Tim Sherwood
Kumbukumbu muhimu za
Sherwood.
Alikuwa nahodha wa klabu ya Blackburn Rovers iliyoshinda
ubingwa wa ligi kuu ya uingereza mwaka 1995.
Alicheza Watford,Norwich,Spurs,Portsmouth na Coventry city.
Alicheza mechi 3 katika maisha yake ya soka kwa upande wa
timu ya taifa ya Uingereza.
Kumbukumbu ya kuvutia
Mechi yake ya mwisho akiwa kocha wa Spurs aliifunga Aston
Villa kwa 3-0 mei 11 2014.
0 maoni:
Chapisha Maoni