Na Hosea Mchopa #UO 1

Barcelona wakishinda mechi zote mbili dhidi ya Manchester City watatinga hatua ya robo fainali kwa mara ya nane mfululizo

#hii ni kwa ajili yako



Klabu ya Manchester City inamtihani mkubwa kuweza kuondoa ile aibu ya miaka ya karibuni ya klabu za uingereza kushindwa kushindana na klabu kubwa katika mashindano makubwa barani ulaya..

Kikosi cha Man City kina kumbukumbu mbaya ya kipigo walichopata cha jumla ya goli 4-1 na kutolewa na Barcelona katika msimu uliopita.

Sergio Aguero' kun' mshambuliaji hatari wa klabu ya Manchester city anaamini kuwa ni mechi mpya kwa pande zote mbili na haitakuwa sawa na mwaka jana.Huku mchezji mwingine wa Man City Samir Nasri akiamini ni waktai sahihi wa klabu hiyo kutengeneza historia.

Wilfred Bonny atacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Barcelona akiwa na Manchester City.
Pia ataanza mchezo wake wa kwanza tangu arejee kutoka katika kombe la mataifa Afrika ,jumamosi alikaa benchi wakati City ilipoibamiza Newcastle goli 5-0.

Luis Suarez akizidi kujitahidi kuendana na mfumo mzima wa Barcelona atacheza mechi ya kwanza katika ardhi ya Uingereza tangu ahamme klabu ya Liverpool.Kocha Enrique amesema mchango wake ni mkubwa na ni mmoja ya wachezaji waanzilishi mashambulizi katika timu yake.


Gerard Pique beki mahiri wa klabu ya Barcelona anamini huu ndio mchezo muhimu wa mwaka mpaka sasa.

Klabu ya Barcelona ilishinda michezo 11 katika michuano yote kabla ya Malaga kuharibu kwa kuichapa Barca kwa goli 1-0.

Lakini Gerard Pique amesema unapochezea klabu kubwa na kucheza mechi kila wiki huwezi kufikiria kuhusu kilichopita unawaza kuhusu mchezo ujao.

mchezo mwingine usiku huu ni kati ya Juventus wakiwaalika Bor Dortmund

24 Feb 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top