Na hosea Mchopa

Nikikumbuka michano ya Profesa Jay kwa lugha ya Kiswahili akipanda na kushuka kwa nidhamu ya muziki halisi.Akitamka neno kwa upekee ili ajenge mtindo wake katika jamii.Ni binadamu gani angechoshwa na ladha zake kama angefika katika anga za kimataifa kwa utamu wa lugha ya Kiswahili.


Yuko wapi Jay Mo akiziadhibu midundo ya P Funk ‘Majani’ hatujamsikia harakati katika muziki wa kimataifa.Leo hii hata Mwana FA huyu sio kabisa mimi ninayemuhitaji akipambana na darasa kwenye chati za muziki wa Nyumbani.AY pekee anafariji wakongwe sasa anauwezo hata wakutamka anataka kufanya kazi na wasanii wa daraja la kwanza marekani.
Jay Mo na Mchizi Mox

Dapo Oyebanjo  D Banj leo hii ana uwezo wa kusimama mbele ya dunia na kujitapa kuwa ameishi katika kiwanda cha muziki kwa miaka 10 na anajivunia kwa alichokifanya.Amefanya muziki katika hadhi ya chini Nigeria na kufikia anga za kimataifa.

Ana mafanikio makubwa ni moja wasanii 20 Afrika wenye pesa ndefu na wenye ushawishi mkubwa.Safari yake hawezi kuisumulia peke yake wengi tumemuona alivyojitahidi  kupigana katika anga za kimataifa.Leo hii Lady Jay Dee,Afande Sele,Juma Nature wasanii ambao wamefanya muziki kwa muongo mmoja wanatamani kufika hapa.Lakini leo bado ni wasanii wachanga katika anga za kimataifa.

Mdau wa Bongo Fleva kutoka chuo kikuu cha Jordan Morogoro Michael Dachi ambaye naye ni msanii wa bongo fleva.Anasema inaumiza wasanii wengi wa zamani ambao ndio walikuwa na ladha za kipekee zenye uasilia wa Bongo Fleva wengi hawana cha kujivunia nje ya mipaka yetu.Msanii gani wa Nijeria angeweza kusimama na kupambana na ladha za Juma Nature kama angekuwa yupo kimataifa.

‘Kibao changu  cha kwanza kilitoka mwaka 2004.Albamu yangu ya kwanza niliitoa mwaka 2005 na kila mara nilisema nilikuwa mburudishaji na niliomba kuwa nitakuwa msanii mkubwa kutoka nje ya afrika.Nitakuwa mfanyabiashara ,unaajua kila mara nina ndoto tofauti’.Dbanj akieleza historia yake ya muziki.
Msanii wa Nijeria Dbanj


Hapa Dbanj ananionesha jinsi gani yeye hakuta kuwa kinara wa Lagos pekee hayakuwa malengo yake makubwa.Yeye alikuwa anawaza kuja kuwa kinara katika muziki wa Afrika tena huku unia ikimshuhudia.Wasanii wetu wengi wao wanatosheka wakiiteka mikoa 26.wakiskika Kenya wanaona tayari wao ni wa kimataifa.

Ninapohesabu baraka ninaona ni safari nzuri sana katika miaka 10 ya muziki wa Dbanjo.Dbanjo mwaka jana anasema kuwa ndio sehemu kuu katika maisha yake yote ya muziki.Alihutubia katika benki ya dunia Tedex hapo moyo wake uligusa sehemu ya pekee.   
Msanii Dbanj

Dbanjo muziki umeshamlipa sana sasa hivi anafurahi anapokuwa balozi wa vijana wengi wa Kinaijeria yuko tayari kujitoa kwa wengine.Naona giza kwa wasanii wetu wengi ukimwacha Ambwene Yesaya AY ambao wametoka mbali kuweza kupata nafasi ya kimataifa kueleza muziki wa bongo walikoutoa.

Lady Jay Dee alifika katika anga za kimataifa lakini muda mfupi tu hakuweza kuendelea kupambana huko.Tunatamani wakongwe wa Bongo Fleva wanoujua muziki wetu wangekuwa hata watano (5) katika anga za kimataifa tungeionesha dunia muziki wa bongo fleva ni muziki uliopiganiwa usiku na mchana kufika hapa.


Inasikitisha hatua zao nyingi zimepotea wakAti tunaziona leo hii wanakumbuka ya jana,hawaishi kukumbusha walivyoitawaal jana.Simaanishi kuwa kosa ni lao hapana inawezekana mfumo wa muziki ulikuwa bado hujajengeka.Lakini bado haitoshi kuacha kuongelea jambo linalogusa kama hili nani hatamani kuona wakongwe wetu leo hii wakitikisa Duniaa kama Dbanj.

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top