#News room
Mkutano wa mawaziri wa fedha kutoka nchi zinazotumia sarafu
ya Yuro, ambao ukikua ukijadili hali ya kiuchumi inayojiri nchini Ugiriki
ulidumu kwa masaa machache tu Jumatatu Februari 16 na kumalizika bila hata
hivyo kufikia maelewano.
Lakini jinsi hali
inavyokwenda ndivyo muda uliyotolewa kwa kuikoa Ugiriki unavyofikia kikomo.
Mradi uliyotolewa na nchi
zinazotumia sarafu ya Yuro ulionekana na Ugiriki kuwa "haufai" na"
haukubaliki", kwani ilikua suala la kuendelea na mpango wa
misaada kwa sasa. " Katika
mazingira haya, makubaliano yoyote hayawezi kufikiwa kwa leo",
Ugiriki imeongeza kusema.
Waziri wa Fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis, alionya kuwa Ugiriki iko katika hali ya hatari kiuchumi.
0 maoni:
Chapisha Maoni