Na hosea Mchopa #UO 1

Manchester united walipambana na Preston North Ends katika mchezo wa FA katika mchezo ambao wenyeji Preston walilala kwa goli 3-1.

Mbele  ya mwamuzi Phil Dowd  mashabiki 21,348 walilolipia kiingilio walishuhudi HerreRa dakika ya 65 ,Fellain dakika ya 72 na nahodha Wayne Rooney ‘WAZA’ dakika ya 82 wakipachika magoli kwa upande wa united.

 Alikuwa ni Laird dakika ya 47 ndiye aliyefungua kalamu ya magoli na goli pekee kwa Prestoni

Dondoo muhimu za dimbani

Manchester United walitawala mchezo kwa asilimia 65 kwa 35 za Preston

Pamoja na Preston kupiga mashuti 14 waliwazidi shuti moja tu Manchester united waliopiga mashuti 11 katika mashuti yaliyolenga golini.Preston walilenga mara 6 wakati united mara 5.

 Kiungo wa Manchester united Ander Herrera alicheza mechi yake ya tatu ndani ya miezi mitatu.

4-1-2-2-1 ni moja ya mifumo kocha Van Gaal aliyotumia katika mechi ya Manchester united dhidi ya Preston North end.

Ilikuwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1972 Manchester united kucheza katika dimba la Preston katika mchezo wa mashindano.

PAMOJA NA KUFUNGWA KOCHA WA PRESTON ALITOA KALI YA KIPEKEE

Kocha wa Preston Simon Grayson


‘Tulitengenza baadhi ya nafasi nzuri katika muda na wachezaji wanaweza kuamka asubuhi wakijipongeza kwa kitu walichokifanya.

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top