Na hosea Mchopa #UO 1
Mbele ya mwamuzi Cuneyt Cakir mashabiki wa soka walishuhudia
matukio ya aina yake katika usiku wa mabingwa wa ulaya.Katika mechi kali kati
ya Chelsea na Paris Sain German.
Klabu ya matajiri wa ufaransa Psg pamoja na kutawala
mchezo kwa asilimia 54 kwa 46 waliambulia sare ya goli 1-1 na Chelsea.
Alikuwa beki wa Chelsea Ivanovic katika dakika ya 36
alipounganisha mpira kwa kichwa na kufunga goli la 5 kwa msimu huu na kuwapa Chelsea matumaini ya kusonga
mbele.
Mchezaji hatari raia wa Psg Edison Cavan alisawazisha goli
dakika ya 54 na kufanya matokeo yaishe kwa sare ya goli 1-1.
MAMBO MUHIMU YA
KUVUTIA PSG V CHELSEA.
Ibramovic amefunga magoli 7 katika hatua ya mtoano katika
mechi 34 alizocheza
Ivanovic jana alifunga goli lake la 1 katika michuano ya
ulaya tangu mwaka 2013 alipofunga katika fainali ya ligi ya europa dhidi ya
Benfica.
Ediso Cavan amefunga magoli 5 katika mechi 6 na kuisaida PSG
kufanya vizuri katika hatua ya makundi.
Beki raia wa Brazil mzaliwa wa Diadema David Luiz alicheza akiwa amevaa jezi ya PSG akitumikia katika
nafasi ya kiungo dhidi ya timu yake ya zamani Chelsea
..
Kwa matokeo haya bado
yanatoa mwanga kwa pande zote mbili kuelekea mchezo wa marudiano
0 maoni:
Chapisha Maoni