Na Hosea Mchopa #UO 1
Mabadiliko yanaandaliwa na watu ambao walifikiria matokeo
kwa kiwango cha kati.Lakini mabadiliko siku zote yakija huwa yana uwanja mpana
ambao waliyoyaleta hawakudhani kama yanaweza kufika huko.Kama binadamu mwenye
jicho la tatu tunatakiwa kujua kuwa kila kilichobadilika tukitumie sawasawa.
Sasa hivi dunia imeabadilika njia nyingi za mawasaliano
zimeibuka na kurahisisha mawasiliano kuliko wakati wowote ule .Kama tunaweza
kutumia muda mwingi kuwakabili wasanii,wanasiasa na watu maarufu na wakapata
presha kubwa kwenye maisha yao.Hatujafikiria njia nyingine ya kutumia mitandano
hii katika kupambana na mauaji ya Albino.
Takwimu zinasikitisha toka mwaka 2006 karibu Albino 74
wameuawa na 56 wakinusurika kifo huku 11 kati ya hao wakisababishiwa ulemavu.Hii
inasikitisha huku jamii tukiishia kushiriki kutuma picha za miili ya Albino
waliouawa na kuandika jumbe za kusikitisha.
Tatizo la ulemavu wa ngozi ni la kawaida sana katika dunia
ya kwanza.Ni kitu cha kawaida ambacho kinaweza kikamtokea hata mototo wako ajae.Je?
nae unamuandalia masikikitiko kwa nini usibadili jamii ya kitanzania mapema.
Kama unatumia nguvu nyingi kutafuta pesa ili apate huduma
kamili kwa nini usibadili dunia yake pale atakapozaliwa.Akiwa Albino aikute
Tanzania mpya na asiharibike kisaikolojia juu ya ulemavu wake.Akiwa mzima akute
jamii inayowaheshimu Albino na yeye aunge mkono.
Watanzania Huu ukosefu wa pigment katika macho,nywele na
ngozi ni jambo la kawaida kwa wenzetu.Nchini Marekani kati ya watu 20,000 mmoja ni albino na wapo salama
wakipata haki zote stahiki.Tanzania mtu mmoja kati ya watu 1400 ni albino.
Kama watu hutumia mitandao ya kijamii kubadilisha fikra za
watu juu ya mgombea gani wampe kura mwaka 2015.Mavazi gani ukivaa utaonekana ni
mtu unayeenda na wakati kwa nini msibadili watu kuwa kuua Albino ni ukale.Kwa
nini tusijitoe kimasomaso kuuumbua mipango yote ya hatari juu yao.
Kuna watu wengi katika jamii wana imani potofu juu ya albino
na wamezipata katika mitandao ya kijamii wakiamini Albino hawezi kufariki na
kuzikwa.Mtu kama huyu ni rahisi kupandikizwa chuki juu ya albino ambao wapo
wenye uwezo wa kimaendeleo kuliko wewe.
Kutuma picha ya Albino aliyeuawa na kufanikisha kupata
michango mingi katika mtandao wako.Haikuongezee chochote katika maisha yako
wala kukupa umaarufu wowote wenye faiada katika dunia hii iliyoendelea.Hakuna
jambo la busara litakalobadili maisha yako kama kuhesabika mmoja ya wapambanaji
dhidi ya mauaji ya Albino.
Watoto wenye ulemavu wa ngozi Albino wakiwa katika shule ya msingi Mttindo Misungwi
0 maoni:
Chapisha Maoni