#news room
Silaha kali za kivita
Silaha kali bado hazijaondolewa kwenye
uwanja wa mapambano mashariki mwa Ukraine
Majeshi ya Ukraine na ya
waasi wanaoungwa mkono na Urusi bado hawajaziondoa silaha kali kutoka kwenye
mpaka wa uwanja wa mapambano mashariki mwa Ukraine. Silaha hizo zilipaswa
kuanza kuondolewa leo Jumanne.
Silaha kali za kila upande zilipaswa kuondolewa kuanzia leo
kwenye mpaka wa uwanja wa mapambano,kwa mujibu wa makubalinao ya kuyasimamisha
mapigano yaliyofikiwa baina ya viongozi wa Ujerumani, Urusi,Ufaransa na
Ukraine. Kila upande uliashiria hapo jana kuwa utaziondoa silaha zake ikiwa
mwingine nao utafanya hivyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni