Na Hosea Mchopa #UO 1
Mechi hii ilikuwa ni ya mara ya
kwanza kwa Suirez kukutana tena na kipa Joe Hart tangu wakutane Brazil Sao Paulo june 19 .Ambapo Uingereza
ilifungwa goli 2-0 na Uruguay huku Suarez akimtungua magoli yote mawili Joe
Hart kama alivyofanya jana.
![]() |
Luis Suarez akishangilia bao lake baada ya kuitungua City |
#hii kutoka etihad kwa ajili yako
Mshambuliaji hatari wa klabu ya
zamani ya Liverpool Luis Suarez ameweza kuendeleza historia yake ya ufalme kila
anapokanyaga ardhi ya Uingereza baada ya
kuifunga Man city wakiwa nyumbani Etihad kwa goli 2-0.
Ilikuwa ni mechi iliyosubiriwa kwa
hamu na wapenzi wa soka duniani huku Gerard Pique akiamini ni mechi bora kwa
mwaka mpaka sasa.
Ilichukua dakika 16 tu kwa
mshambuliaji hatari wa klabu ya Barcelona Luis Suarez kuweza kutikisa nyavu
mbele ya kipa Joe Hart.
![]() |
Luis Suarez akipachika bao la kwanza la Barcelona |
Suarez akicheza kwa uzoefu mkubwa
dhidi ya timu za uingereza alithibitisha kauli ya kocha Luis Enrique kuwa
mchango wake ni mkubwa katika klabu baada ya kupachika bao la pili dakika ya 30.
![]() |
Luis Suarez akishangilia bao la pili alilofunga akika ya 30 |
Alikuwa Kun Sergio Aguero dakika
ya 69 ndiye aliyeweza kuamsha hisia za mashabiki wa Man city kuwa wanaweza
wakasawazisha mechi hiyo.
![]() |
Sergio Aguero mfungaji pekee wa bao la City alilokwamisha dakika ya 69 |
Katika Mchezo huo Lionel Messi
alikosa penati hivyo kuipa City matumaini ya kuweza kusonga mbele endapo
watapambana vyema Camp Nou.
![]() |
Joe Hart akichza penati ya Lionel Messi |
Gael Clichy alienda nje kwa kadi
nyekundu na kuipa City wakati mgumu wa kuzuia kasi ya Barcelona.
City mechi ijayo watapata faida
kwa kurejea kwa Yahya Toure ambaye anaifahamu klabu ya Barcelona,uwepo wa Silva
na mshambuliaji wa daraja la juu Aguero unaweza ukasababisha maajabu
yasiyofikirika.
#UO FACT
Suarez alifunga goli moja katika
mechi 6 alizokutana na Man City akiwa na jezi za Liverpool..
Sergio Aguero alipiga mashuti
mawili tu langoni lakini alifanikiwa kufunga moja.Wakati Edin Dzeko alipiga
mashuti 6 bila mafanikio.
Katika mechi 2 za mwisho Suarez
alizokutana na Joe Hart amemfunga magoli manne.
Suarez akimtungua Joe Hart akiwa na jezi ya Uingereza nchini Brazil
![]() |
Luis Suarez akimfunga bao kipa Joe Hart katika mechi ya Uingereza dhidi ya Uruguay nchini Brazil |
Sergio Aguero amefunga magoli 11
katika mechi 10 za ligi ya mabingwa zilizopita
Barcelona katika mechi ya jana
walitawala mchezo kwa asilimia 61-39 za Manchester City.Huku wakifanana idadi
ya mashuti yaliyolenga golini kila mmoja alipiga mara 9.
0 maoni:
Chapisha Maoni