Na Hosea Mchopa
Macho yao ni meupe kama wanamatumaini na siku ya kesho,kucha
zao fupi ukiwauliza watakujibu ni watu wa amani hatupo tayari kushambulia.Mimi
siko tayari kuwasubiria waamke nitawaamsha kwa wimbo wa taifa.
Usimwache mwizi aingie ndani kwako mara tatu.Mara ya kwanza ilitosha,mara ya
pili ilikuwa ni nafasi.Mara ya tatu ina maana wewe ni mjinga.Tumewapa jina
jipya wanunuzi wa mboga tukiwasifu kwa ujanja huku tayari wameshatuibia.
Mawazo yakiwa mengi katika kichwa chako ujue una mambo
unatakiwa uyafanye.Ajabu wao ni wepesi kusoma na kucheka ama kulalamika kisho
kukunja gazeti na kuondoka.
Wana jina jipya siku hizi ‘Wadanganyika’,hulikubali na
kucheka kuwa limebuniwa tu kutokana na jina la Tanganyika.Hakuna tafsri mbaya kama
ya kuhisi jibu lisilo na mashiko ukalipa asilimia 100.
Tumeharibika ubongo tunaweka imani kwa mtu kutokana na hela
zake na wenye ubongo ulioshiba tunawaita wapiga kelele.Tumebadilika sana kama
hatujawahi kuwaza juu ya kizazi kijacho.Watukoseao tunawasifu kuwa wana macho
ya makengeza.
Bado wana imani kuwa nchi jirani zinakuwa kwa kasi kutokana
na udogo wa nchi wala si uhodari wao.Hii upelekea kuamini sisi lazima tukue
taratibu kwa kuwa nchi yetu ni kubwa yenye mikoa 26.Uvivu siku zoye huongozwa
na mbinu za ulegevu.
Buddha aliona mbali na kusema “fikra ni kila kitu,kile
unachofikira ndivyo utakavyokuwa”.Tunawaza bado kuwa wale ndio wanainama kwa
masaa kutunga sheria nchi itaendaje.Wale wakiinuka ndio wataendesha nchi
watakavyo na sisi tutazame na kumuinamia anayekubaliwa na wao.
Baadhi ya wachungaji wamakanisa nao wanaelemewa na misaada ya
ujenzi wamakanisa.Wanakubali kuta zilizosimama zije miaka mitano kuwagharimu
kuirudisha Tanzania waliyoizoea.Je watahubiri kwa kujikosoa na kulia machozi ya
damu kuonesha kujutia.
Baadhi ya viongozi wa kiislamu ‘masheikh’ nao wanalazimika
kuwatumikia watu hatari ambao watawafanya waumini wao wasiifaidi nchi yao miaka
ijayo.Heri tunyamaze kimya mana ukimya unalipa.Siku zote ukimya wa wananchi ni
onyo kwa kiongozi.
Kama tumeshindwa kukwepa kwa nini tusiwe wanafiki kwao
tunazidisha ukaribu usio na tija katika hadhi ya wadhifa wetu katika jamii.Tutembee
na ule msemo kuwa sisi ni watu wakutanguliza
wenzetu mbele.Tena hatari ikiwa mbele.
Wataalamu wetu wamekuwa watumwa maarufu wameamua kuharibu
hata mfumo wa matumaini kwao.Sasa ni ngumu kuwatofautisha wao na wale waliokosa
bahati ya elimu.Wamebakiwa na maneno ya jeuri kuwa wanafahamu nchi nyingi
kutokana na umaarufu wao.
Bado hatuna nia ya kuamini uongozi ni nafasi maalumu iliyopangwa
kwa ajili ya kuwatumikia watu.Bado tunaamini kiongozi ni yule aliye na uwezo
mkubwa wa kifedha katika jamii anayewaza kutimiza majukumu yetu kutoka mfukoni
kwake.
Mungu ibariki nchi yangu Tanzania.Maana watanzania wenyewe
hawafahamu hakuna Tanzania bila watanzania.Bado hawana nia ya kuamua kulinda
ardhi kwa ajili ya vitukuu vyao.
0 maoni:
Chapisha Maoni