Na Hosea Mchopa
Wayne Rooney katika sehemu ya maandalizi yake huwa anakwenda
kwa msimamizi maalumu wa vifaa vya michezo.Anamuuliza rangi gani ya jezi
tunavaa,kama ni fulana nyekundu,bukta nyeupe na soksi nyeusi au
nyeupe.Akishafahamu anaenda kulala na kuvuta picha atakavyofunga goli au
kufanya vizuri.
Ni homa ya jiji ambayo haijalishi umekaa upande gani wa
jukwaa la uwanja wa taifa da es salaam.Uwe haujavaa rangi ya kijani au nyekundu
lakini nawe huugua na huitaji daktari mmoja tu mfumania nyavu.Daktari
atakayeleta jeneza uwanjani au atakayewafanya mashabiki waonyeshe ishara ya
kuchinja.
“Ninavutiwa pekee na
ufungaji wa mabao .Sikuvutiwa na kitu chochote kingne.Garry Lineker mchezaji wa
zamani wa Everton kwenye miaka ya 1985-86 na mtangazaji wa michezo katika kipindi
cha Match of the day BBC.Anakata mizizi ya nini watu wanasubiri uwanja wa
taifa.
Nani leo kati ya Emmanuel Okwi na Ami Tambwe wanawaza kama
Gary Lineker mchezaji pekee aliyetwaa kiatu cha dhahabu katika kombe la dunia
mwaka 1986.Vijiwe vingi vya homa ya jiji huwazungumzia wafumania nyavu.Simba
wakijitapa na goli zao 5 wakati Yanga wakikumbuka goli 2 .
Mechi ya Simba na Yanga kwa siku za karibuni imekuwa inaenda
tofauti kabisa na msemo wa Vince Lombard tulivyo inatokana na nini tunafanya na
nini tunacho.Yanga siku za karibuni hata kama ikiwa kwenye kiwango gani
ikikutana na Simba ya kawaida inapata tabu sana kupata matokeo.
Isingekuwa roho mkononi kama leo ingekuwa ni mwaka
2003,mashabiki wa Simba wangevaa jezi lao nyekundu siku moja kabla ya mchezo.Hofu
ingetoka wapi,golini Juma Kaseja akilindwa na Said Sued,Ramadhan Wasso,Boniface
Pawassa na Patric Betwel.
Pluijm anatumia muda mwingi kujiuliza nani awe daktari wa homa
ya jiji.Homa ambayo watu wengi wanatamani iwepo hata mara sita kwa
mwaka.Anakumbukumbu ya sare pekee alipohatika kupambana dhidi ya Simba mara
moja pekee na Simon Muva kumuura dakika za majeruhi.
Pamoja na ubora wa Ndemla kuchezesha klabu ya Simba
akisaidiwa na Jonas Mkude katika ukabaji.Fumbo kubwa ni namna gani watahimili
mikiki ya Telela na Niyonzima kama wakianzishwa kuweza kumfikihisa mipia
Hajjib.Na sio kufikisha tu bali kuleta maafa wanyowaletea katika nani mtani
jembe.Nani gani ndemla atafanya maajabu zaidi ya yale ya kuisaidia Simba
kurudisha mabao 3 didid ya Yanga.
Bahati ya kipekee ni uwepo wa makocha wazawa ambao
wanafahamu homa hii kiundani zaidi.Suleiman Matala akiijua Simba akiwa mchezaji
,kocha wa vijana na novemba 19 2013 akipata nafasi kwa mara ya kwanza kuiongoza
timu ya wakubwa baada ya Kibadeni na Julio kutimuliwa.
Je atamuonesha Goran Kopunivich njia bora ya kuwatumia Messi
na Okwi ili kutifua mbio za Yanga kileleni.Atampa ushauri gani juu ya nani
anastahili kuaminiwa katika safu ya ushambuliaji kwa siku ya leo.
Ni mechi ambayo hatupaswi kumdharau yoyote nani anakumbuka
maajabu ya Juma Awadhi aliyoifanya Yanga mtani jembe.Tusije kushangaa leo
Maguri akiwasumbua sana Canavaro na Vidic kama wakianza pamoja.
Boniface Mkwasa na yeye ni mtu muhimu kwa klabu ya Yanga
uzoefu wake umakini wake kwa wachezaji unaweza ukampa nafasi ya kuipa yanga
matokeo.Chicharito akiwa Manchester united siku zote huwa hakosekani mechi
dhidi ya Chelsea hata awepo nje kwa muda gani.
Mkwasa ni mtu pekee anayeweza kumuonyesha Pluijm kijana
Jeryson Tegete kuwa ni mwiba mkali kwa Simba amefuga karibu mabao 5
alipowavaa.Ijapokuwa hayupo vizuri siku za karibuni.Uwepo wa Mkwasa unaweza
ukaleta ladha zisizotarajiwa kwa kumpa nafasi kijana ngangari Hussein Javu.
Homa hii ya jiji huboresha mikataba na pia huaribu
mikataba.Tanzania hamna soka la kweli ni Simba na Yanga wakati pekee
tunapoamini sisi ni wa kwanza Afrika Mashariki.Mapato yanakuwa mengi,ndio mechi
wachezaji wanapewa marupurupu.
Haya yote yanafanywa kwa lengo moja tu kupata tiba ya homa
la jiji,wanataka mabao yatakayoamsha hali ya klabu.Simba ikishika nafasi ya nne
na kuhitaji ushindi kuanza kukimilia kileleni.Wakati Yanga wakihitaji pointi 3
kujihakikishia ushindi wa vita yao dhid ya Azam na Kagera Sugar.
Wametafuta fukwe nzuri zenye utulivu wakijifua Zanzibar na
Bagamoyo kwa kuwa wanafahamu hii ni mechi itakayoleta homa katika klabu
zao.Homa inayosambaa jiji nzima na hakuna tiba inayohitajika zaidi ya kutikisa
wavu mara nyingi kuliko mwenzako.
0 maoni:
Chapisha Maoni