Na. Hosea Mchopa

Wewe ni nani katika jamii yako na unaipa nini jamii yako inayokuzunguka.Na wala sio wewe umepata nini katika jamii na una nini katika jamii.Fikra ni kila kitu katika siku ya kesho lakini kuwaza hakuwezi kukupa picha ya kesho utashiriki nini.Ni fumbo la karne lenye ukurasa zisizoisha kuzichambua.

Wakati mgumu siku zote hutengeneza jambo jema na la kuvutia katika maisha ya binadamu.Kujitafakari huibuka sehemu pekee ambayo Mungu naamini anatamani kila mwanadamu aipate hii nafasi.Hutufanya kuwa tulioshuka tukitazama juu na kuamini kuna kitu tunahitaji kurekebisha.

Maya Angelou aliwahi kusema nimejifunza watu watasahau ulichosema,watu watasahau ulichotenda,lakini hawatasahau jinsi ulivyowafanya wahisi.Kuna wakati tutasahau walichofanya wakiwa wametangulia mbele za haki.Lakini watu wanaweza wakahisi nini moyoni wakisikia jina lako.

Kujitafakari kwa kina huzaa matunda yaliyo na gharama kubwa sana katika maisha ya binadamu.Matunda haya hugharimu muda,maumivu,tamaa mpya na maamuzi ya kishujaa.Kujitafakari huja baada ya makosa,huja baada ya kupotea njia,huja baada ya kuhisi hatutapita panapostahili.


Ni rahisi sana kupata nafasi hii ya muhimu ambayo inaweza kuweka alama moyoni mwako.Alama ambayo itakufurahisha baada ya kurekebisha au itakuumiza kwa kujua bado unaendelea kukosea.Bahati iliyoje kujitafakari kunaweza kukatokea kupitia wengine.

Nasikia huzuni iliyo kubwa napoona binadamu wanachochea kuni moto huunguzao nyumba ya jirani.Ilihali wao hawana mkataba na siku inayokuja,kinachoumiza hawajapata nafasi muhimu ya kujitafakari.Hakuna ajuayesiku ya  kesho kwa aliyekosa na aliyekamili.

Jamii inaweza ikawa na tafsiri nyingi mbaya juu ya mwanadamu Fulani.Lakini anayeamini fikra ni mali huendana kinyume na tafsiri zao pekee hutaka kutumia ile nafasi kuamini wao pia hawajakamilika.Wao hutumia fursa ile kujionya kuwa sipaswi kujiona bora kwenye kila kitu napaswa kuwa na macho yenye kunionyesha hatari mara nyingi iwezekanavyo.

Sauti ya gharama siku zote haifungamani upande wowote husimama katikati ya pande nne za dunia na kutuliza upepo wa kus na kas.Kwa nini tusitumie makosa waliofanya wenzetu kujitafakari na kuamua kesho ipi idondokee machoni petu.

Kesho yetu nani anaidhamini kwa kuhukumu,kulikoni kusahihisha ili wasiopata muda wa kujitafakari wasafiri nasi.Walikosea wametangulia hatuko nao tena katika ulimwengu huu ambao wametokea.Lazima tuongee kuhusu wao kwa sababu walikuwa watu wakubwa katika jamii yetu lakini tunaitumia nafasi hii vyema kutengeneza kesho yetu.

Rafiki yangu alikuwa mlevi wa kupindukia na alisifika kila kona alipopita.Katika maisha yake ya nyuma alidharau walevi kulikoni watu wowote wafanyao maovu katika jamii.Yeye hakutumia nafasi kutafakari siku zake za usoni juu ya sababu zipelekeazo ulevi.Wala hakuwahi kujitafakari nyendo zake zipo njia gani.

Alipofika chuoni akajichanganya na mwishoe akaangukia katika ulevi uliopindukia.Akawa kiumbe cha ajabu hajui alichofuata chuoni wala jamii yake inahitaji msaada gani kutoka kwake.Baadaye akapata mkasa uliomfanya atafakari juu ya ulevi,unampa nini na unamfanya awe nani katika jamii.

Akanipa funzo kubwa sana kipindi cha nyuma hakutumia nafasi ya athari za walevi wengine kujitafakari yeye.Yeye aliishia kuwadharau na kuwalaumu kitu ambacho akikumweka karibu na Mungu ili aweze kupanda matunda yenye gharama.Leo hii ameitumia nafasi vyema ya kujitafakari kwa na ameachana na ulevi.

Na amepata nguvu ya kuweza kukomboa waliothika na ulevi.Walikuwa viongozi wakubwa na waliishi katika jamii yetu kinyume na matarajio yetu.Lakini tunaangalia mgawanyo wa muda wetu katika kunung’unika kwa waliyotenda na kujitafakai upya kwa njia walizopita.


Maisha yana mwisho tena usiojulikana kwa kila mmoja,hatupaswi kutumia muda mwingi kulaumu visivyo jibu.Tutumie ule muda kujitafakari na kuonyesha njia ya kupita ili wakati wako ukifika watu wajae na hisia za ulivyowafanya waone kuna kitu cha pekee ndani ya moyo wako.

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top