Na Hosea Mchopa #UO 1

4-3 ni pumzi inayoshikilia soka kwa hivi sasa.Unajua kwa namna gani Messi akichungulia gazeti la michezo la Marca akiiona 4-3 anavyowaza kuongeza juhudi.Je umewahi kuwaza kijana wa Madeira Cristiano Ronaldo anavyowaza kuipigania.

Pumzi zao zimetikiswa na binadamu aliye  na damu ya kibrazili.Nchi iliyobarikiwa warembo wenye majina ya kuvutia Ana Amelia,Ana Lucia,Ana Livia,Alidaci.Turudi kwenye mstari wetu.

Huyu ni mkongwe mwenye miaka 74 aliyechaguliwa na shirikisho la takwimu na historia ya soka (IFFHS)kuwa mchezaji bora wa karne mwaka 1999.
Perola Negra O Rei Pele



Huyu si mwingine ni Edson Arantes do Nasciamento ‘ O Rei Pele’  au Perola Negra anaposahau kumweka Ronaldo daraja moja na Booby Moore,Boby Charton na George Best.Kamweka Messi tu tena na wakongwe kama Zico na Rivaldo.

Kauli ya Pele juu ya Ronaldo na Messi huwa na nguvu ya aina yake katika ulimwengu wa soka.Kumbuka Pele ni mchezaji anayeheshimika kwa kutupia magoli 1281 katika mechi 1363.

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wapo kwenye ulimwengu wa ushindani mkubwa katika soka.Ulimwengu wao unaanza ndio unafuta wa Suarez,Neymar,Bale,Benzema,Aguero,Rooney na wengine.

Hivi sasa dunia nzima inageukia nchi ya Hispania kuangalia wanaume wakipambana katika mechi yenye mvuto kwa sasa El Classico.Mechi ambayo inatoa hamasa kubwa sana katika mbio za ubingwa ukizngatia wao ndio washindani wakuu.
Cristiano Ronaldo CR7

Cristiano Ronaldo alianza msimu huu kwa hamasa kubwa na ya kutisha baada ya kufunga mabao 25 katika mechi 14.Lakini Tangu mwaka 2015 uanze amekuwa chini ya kiwango kwani michezo minne ndani ya mwaka huu alishindwa kupiga shuti lilolenga kwenye goli.Na amefunga mabao 5 tu.

Mwaka 2015 umeharibu rekodi yake aliyoweka  miezi 15 iliyopita ya kufunga michezo ya Bernabeu.Ilikuwa katika mchezo dhidi ya Espanyol walishinda bao 3-0 lakini Ronado hakufunga bao lolote.

Kuna taarifa kuwa Ronaldo anatarajiwa kukwepa vyombo vya habari ili kuendelea kutuliza akili.Kwani vyombo vingi vimekuwa vikihitaji kumchomekea swali la mahusiano yake na Irina Shayk.Ambaye tayari amechafua hali ya hewa baada ya kusema kilichosababisha aachane naye kupitia Holla magazine.

Msumari wa Pele unaweza ukawa umetikisa pumzi na hasira za Ronaldo kutaka kuonesha ulimwengu kuwa yeye ni bora.Naye Lionel Messi pumzi zake zitatikiswa na mafanikio ya Ronaldo kwa kuhitaji kufanya zaidi.Ili kushindana katika kuongeza ballon dor  ya 5.

Lionel Messi katika mechi 17 za Barcelona ametupia magoli 20 na akitoa pasi za goli 12 akikimbia kwa kasi ya ajabu mwaka 2015.

Pia Lionel Messi amepata nguvu ya ajabu kutokana na maelewano mazuri yaliyopo kati yake na wachezaji wenzake Neymar Jr na Luis Suarez.Huku Madrid hali ya Gareth Bale na Ronaldo ikiwa si shwari kwa kulaumiana juu ya ubinafsi.
Lionel Mess La Pulga


Akiwa na hali ya ajabu na klabu kiujumla wakiwa wameshinda mechi 9 kati ya 10 zilizopita.Kauli ya Pele itakuwa imetikisa pumzi zake na anajua anatakiwa kujitahidi zaidi kabla ya Ronaldo hajarudi katika kiwango chake.

Pele amechochea moto wa Ronaldo kuhitaji kuchukua tuzo ya Ballon Dor   a 4 hili iwe 4-4.Kuelekea mchezo huu hakuna anachohitaji  zaidi ya kufanya maajabu.

Kama Ronaldo ataisadia klabu yake kushinda dhidi ya Barcelona atakuwa ameishuhudia rekodi ya aina yake.Real Madrid mara mwisho kushinda mechi 3 mfululizo dhidi ya Barcelona ilikuwa ni mwaka 1978.

Ronaldo amefunga mabao 8 katika michezo 7 waliyosafiri kwenda Nou Camp.Je atatamba tena mbele ya Messi.Au mechi hii itamtengenisha kabisa na mashabiki wa Madrid waliompigia kura awe anaanzia benchi.

Pamoja na kuhitaji ushindi wa pointi 3 za kuwezesha klabu zao kuendeleza vita za kuchukua la liga.Hakuna siri Ronaldo na Messi wapo katika mashindano ya tuzo ya mchezaji bora wa dunia.Messi akiwa ana tuzo 4 na Ronaldo 3(4-3).


Perola Negra hajafanya kosa ametikisa pumzi zao mapema kabla ya El Classico.Hakuna asiyehitaji kuona El Classico inakuwa mechi ya Ronaldo au Messi.Uso huwa mkali chuki ikitanda njia moja tu ya kuleta tabasamu ni mafanikio.Ni la Pulga (Messi ) au CR7 (Ronaldo).
22 Mar 2015

0 maoni:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top